Home News SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA

SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA

845
0
Serikali imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza  nyavu aina ya makokoro 35 , makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro
 
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo,Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi  Abdalah Ulega  amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali  imekua ikipoteza kiasi kikubwa cha mapato kutokana na uvuvi huo.
 
“Hatuna utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi hii, Tanzania ndio nchi yenye  sehemukubwa  yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado tunaagiza samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa litakuwa historia kwa vizazi vijavyo” amesema Ulega
 
Kwa  upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira  alisema uwepo wa bwawa hilo umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa ni wakati wa wananchi kuwa walinzi kwa kila mmoja ili kutokomeza uvuvi haramu.“Hebu leo amueni kabisa kwamba  biashara ya samaki ndio mfumo wa maisha yenu, Ninyi mkifanya hivyo sisi hatutahitaji kufunga hili bwawa , wakati wote tutahitaji kuongeza kizazi cha samaki na kuleta wataalamu kupima kiwango cha samaki tulichonacho” alisema Mghwira
 
 Kwa upande wake Dismas Gondwe mkazi wa kijiji cha kigongo kata ya Lang’ata amesema  uvuvi haramu katika bwawa hilo unatokana na kukosekana kwa utaratibu maalumu unaowaelekeza  wavuvi kuendesha  shughuli zao katika bwawa hilo.
 
Gondwe ameiomba serikali kuwawezesha  wavuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu zana  harali ambazo serikali inazitambua.

 

Naibi Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro kuhusu serikali kutokumuonea huruma mtu yoyote ambaye atajihusisha na shughuli za uvuvi  haramu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
_DSC9916
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.
_DSC9935
 Naibi Waziri Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Abdallah Ulega (wakwanza kulia) kwa kushirikiana na  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira na  Mkuu wa wilaya ya Mwanga Aarron Mbogho wakiteketeza zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
_DSC9867
 Sehemu ya wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
_DSC9949
Zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu zikiteketezwa