Home News SERIKALI KUTOA MWONGOZO WA USAMBAZAJI KOMPYUTA SHULENI

SERIKALI KUTOA MWONGOZO WA USAMBAZAJI KOMPYUTA SHULENI

1520
0

Serikali imesema inatarajia kutoa mwongozo wa utaratibu wa kusambaza kompyuta na vifaa vyake katika shule za msingi na sekondari ili kuwezesha vifaa hivyo kutambuliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu sahihi  kwa shule ambazo  zitakuwa zimepatiwa vifaa hivyo.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya TEHAMA yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo amesema kwa sasa ni vigumu kwa serikali kujua ni shule ngapi zenye kompyuta ama taasisi zinazotoa misaada ya kompyuta shuleni.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza na washiriki wa mafunzo ya TEHAMA (hawapo Pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam ambapo amewataka washiriki hao kutumia maarifawaliyoyapata katika kuboresha Elimu

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakaa pamoja na Ofisi ya Rais Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa ili tuweze kuweka mwongozo ambao utawezesha serikali kutambua taasisi zote zinazojishughulisha na usambazaji wa kompyu takatika shule pamoja na kutambua shule zilizo na kompyuta ili iwe rahisi kuziratibu”amesema Prof. Mdoe.

Akizungumza na Walimu walioshiriki mafunzo hayo amewataka kuhakikisha wanatumia maarifa waliyoyapata katika kuboresha elimu na kuimarisha utendaji wa kazi ili kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Pius Joseph amesema mfuko wa Mawasiliano kwa wote ina jukumu la kuhakikisha ina ziunganisha shule zote za msingi na sekondari katika mtandao wa inteneti, pamoja na kutoa vifaa na mafunzo kwa walimu wanaofundisha masomo ya TEHAMA .

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akimkabidhi cheti cha kumaliza mafunzo ya TEHAMA mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

 

 Mfuko  huo wa Mawasiliano tayari umetoa  mafunzo yaTEHAMA kwa  walimu 578 kutoka mikoa yote ya Tanzania pia umetoa kompyuta 425 kwa shule za msingi,  komputa 1250 kwa shule za sekondari  na kuwa vifaa hivyo vimetolewa katika  kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018.