Home Michezo SIMBA NA YANGA VITANI TENA KWA NYOTA HUYU..

SIMBA NA YANGA VITANI TENA KWA NYOTA HUYU..

157
0

 

Kiungo wa APR, Iranzi Jean-Claude amefungua mlango klabu za Yanga na Simba na nyingine za Afrika Mashariki zinazotoka kumsajili.
Kiungo huyo amewahi kucheza katika klabu ya Mvk ya Slovakia baada ya kuondoka APR, lakini alipokuwa nchini Slovakia alipata matatizo ya kifamilia na kumfanya avunje mkataba na klabu hiyo.
Meneja wa mchezaji huyo Gakumba Patrick alisema Tanzania ina klabu mbili Yanga na Simba,  zimeonyesha nia yakuhitaji huduma ya mchezaji huyo, lakini Kenya nako kuna timu zimeonyesha nia.
“Kijana alikuwa anapenda aje acheze Tanzania, lakini Tusker ya Kenya nao wamenambia wanamtaka tunaenda katika mazungumzo kuwasikiliza kuona inakuaje, lakini kikubwa maslahi tutaaangalia,”alisema.
Hata hivyo nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa na Rwanda na klabu ya APR anatakiwa na klabu ya Saint George ya nchini Ethiopia.