Simba Yambwaga Nyota Huyu Wa Kimataifa

0

Mlinzi wa kimataifa wa Simba SC kutoka nchini Zimbabwe Method Mwanjali ameachana na klabu ya Simba SC yenye masikani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam. Mwanjali ambaye ni nahodha wa Simba ameachwa katika dirisha hili dogo la usajili na tayari benchi la ufundi la klabu hiyo sambamba na kamati ya usajili wapo mbioni kumsajili mlinzi mwingine mwenye uwezo mkubwa na uzoefu wa mechi za kimataifa yakiwa maandalizi kwa ushiriki wao katika kombe la Shirikisho mwakani.

Sababu za kumuacha Method Mwanjali ni majeruhi ya mara kwa mara kitu ambacho kinamfanya kushindwa kuutumikia vyema mkataba wake na klabu hiyo kwa asilimia kubwa . Mkono wa kwaheri kwa Mwanjali ni nafasi kwa wekundu hao wa Msimbazi kupata fursa ya kusajili mchezaji mwingine wa kimataifa ili kutimiza idadi ya wachezaji saba!.

Wakati huohuo ujio wa straika mpya kutoka Zambia Jonasi Sakuhawa mwenye umri wa miaka 34 ambaye aliwahi kuvichezea vilabu vya TP Mazembe na Zesco United anaweza kufungua milango ya kutokea kwa mrundi Laudio Mavugo aidha kwenda nje ya Simba kwa mkopo au kuvunjiwa mkataba wake unaokwisha mwakani.

Simba wapo katika maandalizi makali ya kukisuka kikosi chao tayari kwa michuano ya kombe la Shirikisho mwakani, ASFC na duru la pili la mzunguko wa ligi kuu nchini bila kusahau michuano ya kombe la Mapinduzi.

Ujio wa bilionea Mohamedi Dewji kama mmiliki wa timu kwa asilimia 50 baada ya wakali hawa wa Msimbazi kuingia katika mfumo wa hisa, umeanza kuonesha cheche zake kwa kuanza kurekebisha kikosi na mambo mengi e yakiutawala .

987 total views, 4 views today

Facebook Comments
Share.

About Author