Home Michezo SIMBA yaweka Mezani Mkataba wa Ngoma

SIMBA yaweka Mezani Mkataba wa Ngoma

155
0

WAKATI kesho Jumatano straika, Donald Ngoma akisubiriwa kutua nchini akitokea kwao Zimbabwe, tayari uongozi wa Simba umeshamuwekea mezani mkataba wa miaka miwili.

Ngoma ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Yanga ambayo tayari amemaliza mkataba, msimu ujao anaweza kuvaa jezi za Simba kutokana na timu hiyo kuonesha nia ya dhati ya kuihitaji saini yake.

Mzimbabwe huyo aliyejiunga na Yanga misimu miwili iliyopita, tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na Simba huku ikitaarifiwa kwamba yamekwenda vizuri.

Chanzo cha ndani ya Simba, kimesema kuwa baada ya kuwa na asilimia kubwa ya kumnasa Ngoma, tayari wameshaandaa mkataba ili akitua tu asaini.

“Ni kweli Ngoma tunamuhitaji na tayari tumeshaongea nae kila kitu kimekwenda sawa, alisema atawasili baada ya kumalizika kwa Sikukuu ya Idd,” kilisema chanzo hicho.