Home News TAFITI NI SULUHISHO LA CHANGAMOTO KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJ

TAFITI NI SULUHISHO LA CHANGAMOTO KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJ

1736
0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandishi Dkt. Eliakimu Chitutu, akiwaonyesha waandishi wa habari nakala za mapitio za mpango kabambe wa kilimo cha uwagiliaji.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mhandisi Dkt. Eliakimu Chitutu, akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake takwimu zinazoonyesha eneo la kilimo cha umwagiliaji nchini.

, Kaimu Mkuregenzi  Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mhandisi Dkt. Eliakimu Chitutu akiongea na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali katika sekta ya kilimo, hususan kilimo cha umwagiliaji.                           xxxxxxxxx xxxxxxxx

  Mwandishi Maalum.
Dar es Salaam
Imeelezwa kuwa tafiti mbalimbali zinazofanywa na wataalam katika eneo la kilimo cha umwagiliaji zinasaidia  katika kupatikana kwa suhulu na kutatua changamoto za uwekezaji katika sekta hiyo.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Dkt. Eliakimu Chitutu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Chitutu alisema kuwa tafiti hizo zinaweza kusaidia kuishauri Serikali katika kusimamia miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na matumizi bora ya maji kwa wakulima.
Aliongeza kwa kusema kuwa, tafiti hizi zinaweza kusaidia kuongeza  ufanisi katika matumizi ya maji.  “ Skimu nyingi zinatumia njia za asili kama mifereji na sisi tunahamasisha wakulima kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo cha umwagiliaji kama vile kilimo cha matone yaani Drip irrigation.” Alisisitiza Chitutu.
Chitutu amesema kwa sasa Tume ya Umwagililiaji inafanya tafiti mbalimbali katika mikoa ya Dodoma, Iringa na Morogro kwa kushurikiana na wadau wa maendeleo kama vile  Shirika la tafiti kutoka Japan ambalo linalenga katika kuangalia tija ya maji katika skimu ya umwagiliaji  ya Lower Moshi.” Alisema.
Akiongelea Mipango ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,  Mhandisi Chitutu alisema kuwa Tume imekuwa ikiendelea na ujenzi wa skimu za Umwagiliaji kadri ambavyo pesa zimekuwa zikipatikana  na imeweza kufanya upembuzi yakinifu, ukarabati, maboresho na upanuzi wa skimu nyingi za umwagiliaji nchini.
“Maendeleo ya Umwagiliaji yameweza kufanyika kwa pesa za ndani na pesa za nje  toka kwa wadau wa mendeleo, tunahitaji  takribani kiasi cha Sh. Bilioni 592 kwa mwaka kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa skimu na  mundombinu ambayo haijakamilika ili kufikia lengo kuu la  kuongeza eneo la umwagiliaji  kufikia hekta   milioni moja (1,000,000) ifikapo mwaka 2035,.” Alibainisha.
Awali, Mhandisi Chitutu alieleza kuwa Tanzania ina eneo lenye ukubwa wa Hekta Milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambapo kati ya hizo, hekta milioni 2.3 zina uwezo wa juu wa kumwagiliwa  na hekta milioni 4.8 zina uwezo wa kati ambapo hekta milioni 22.3 ndizo zimendelezwa mpaka June 2018. “Kama mnavyofahamu kilimo cha Umwagiliaji ni Kilimo cha uhakika na uzalishaji katika eneo linalomwagiliwa kwa sasa unachangia asilimia 24 (24%) za chakula nchini, tunategemea mchango huu utaongezeka kadri tunavyopanua eneo la umwagiliaji.” Aliongeza Chitutu.