TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA ELIZABERTH MAYEMBA

0

Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mwanachama wake,Elizaberth Mayemba kilichotokea jana  jioni huko nyumbani kwake Tabata kwa Swai.

TASWA imestushwa na kuhuzunishwa  sana kutokana  na kifo hiki cha  Elizaberth ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa unahitajika sana.

Waandishi wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka Elizaberth kutokana na ucheshi,kujituma na  uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa mfano kwa waandishi chipukizi.

TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa habari na kuwatakia moyo wa  subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.

Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. TASWA ipo pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Juma Pinto
Mwemyekiti TASWA
Facebook Comments
Share.

About Author