Home News TATU MZUKA FOUNDATION WATOA TSH. MILIONI 20 KUCHANGIA UKARABATI WA WODI YA...

TATU MZUKA FOUNDATION WATOA TSH. MILIONI 20 KUCHANGIA UKARABATI WA WODI YA WATOTO JKCI

1052
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi pamoja na watoto wenye magonjwa ya moyo wakipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Foundation kwa ajili ya kufanikisha ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Tatu mzuka Foundation wametoa hundi ya shilingi milioni 20 kufanikisha lengo la Rais Magufuli la kuwa na Wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wawakilishi kutoka kampuni ya Tatu Mzuka Foundation walipotembelea taasisi hiyo na kuona maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Tatu mzuka Foundation wametoa hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa wodi ya wototo itakayokuwa na vitanda 32 pamoja na chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa watoto

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani (wapili kushoto) na Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Godwin Sharau wakiangalia hundi ya shilingi milioni 20 iliyotolewa na kampuni ya Tatu mzuka Foundation kwa ajili ya kufanikisha lengo la Rais Magufuli la kuwa na Wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo.
Baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 20 wakati kampuni ya Tatu Mzuka Foundation walipotembelea taasisi na kukabidhi hundi hiyo kufanikisha lengo la Rais Magufuli la kuwa na Wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo
Daktari Bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akielezea namna upasuaji wa moyo kwa watoto unavyofanyika wakati wa ziara ya wawakilishi kutoka kampuni ya Tatu Mzuka  Foundation walipotembelea taasisi hiyo na kuona maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Tatu mzuka Foundation wametoa hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa wodi ya wototo itakayozinduliwa Desemba mwaka huu. (PICHA NA: GENOFEVA MATEMU – JKCI)