Tetesi “Hazard amalizana na Madrid na ameshapata nyumba” - The Choice

Tetesi “Hazard amalizana na Madrid na ameshapata nyumba”

0

Habari kubwa leo Uingereza na Hispania ni ya kumhusu Eden Hazard. Ripoti zinasema tayari Real Madrid wameshapiga hatua zaidi kuinasa sahihi ya nyota huyo ambae inafahamika ni target yao ya muda mrefu.

Inasemekana Real Madrid tayari wameshafanya mazungumzo ya awali na Eden Hazard na kila kitu kimeenda sawa, kinachosubiriwa kwa sasa ni Chelsea kutaja kiasi wanachotaka.

Real Madrid ni kati ya vilabu ambavyo ni ngumu sana kuvizuia vinapomuhitaji mchezaji wako, na mchezaji wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand amesema kama Madrid wanamtaka Hazard ataenda.

Nguvu kubwa ya pesa waliyonayo Madrid lakini pia heshima yao katika soka ni kubwa kuliko Chelsea na ni kati ya mambo ambayo yanaweza kumvutia zaidi Eden Hazard kuniunga na miamba hiyo ya Hispania.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alikuwa akimhitaji Hazard tangu hajapewa ukocha mkuu Real Madrid. Taarifa zinasema kwamba Hazard ameshapata hadi nyumba ya kuishi katika jiji la Madrid.

Hazard amekuwa mhimili muhimu sana kwa kocha Antonio Conte haswa kutokana na mfumo wake wa 3-4-3 na kuondoka kwake litakuwa pigo kwa timu ya Chelsea na mashabiki kwa ujumla kwani Hazard ndio kipenzi chao.

Facebook Comments
Share.

About Author