TETESI ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA MAY 27/2017

0
(SIMBA)
Zikufikie habari njema wewe shabiki na mpenzi wa klabu ya Simba uliyekuwa na wasiwasi juu ya mchezaji Abdi Banda ambaye taarifa zake za Kugoma Kuongeza mkataba klabuni hapo zilienea kipindi fulani kuwa mambo huenda yakakaa sawa na beki huyo akaendelea kucheza Simba msimu Ujao.
Hii inakuja mara baada ya Banda kuithibitisha kufanya mazungumzo na Mfadhili wa timu hiyo Mo Dewji, amesema “Nimeshazungumza na MO na baada ya kumalizika mchezo wetu wa fainali (Kombe la Shirikisho) yetu na Mbao, Jumapili au Jumatatu nitakwenda kuonana naye tena,”
(YANGA)
Kulingana na klabu ya Yanga kutajwa kuwa kama mambo yataenda kama yanavyoenda basi tuwategemee wachezaji Ibrahim Ajib, Kiungo Jonas Mkude na Mohammed Ibrahim maarufu kama Mo Kujiunga na Yanga Msimu Ujao.
Kinachosubiriwa na Ripoti ya Kocha George Lwandamina, Ajib na Mkude wamekuwa wakitajwa Yanga kwa muda toka katikati mwa msimu huku mchezaji Mo Ibrahim akitajwa Kumvutia sana Lwandamina.
(YANGA)
Klabu ya Yanga imesikia fujo zinazofanywa na Singida United kwenye usajili wa wachezaji tangu ilipopanda daraja na kurejea ligi kuu bara na pia imepata taarifa kuwa wapinzani wao wa Jadi,Simba tayari wameshamnasa nahodha wa zamani wa Azam FC,John Bocco Adebayor lakini Mjumbe wa wa kamati yake ya utendaji,Salum Mkemi amesema wao kama Yanga hawatishwi wala hawanyimwi kabisa usingizi na jambo hilo.
Akiongea kutoka Arusha alikoambatana na kikosi cha Yanga kilichowasili jijini humo jana Ijumaa kulitembeza kombe lao la ubingwa pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC,Mkemi amewataka mashabiki wa Yanga kutulia na kuacha uongozi ufanye kazi yake kwa maelekezo ya kocha wao Mzambia,George Lwandamina Chicken.
Amesema Yanga ni timu kubwa na inaweza kuchukua/kusajili mchezaji yoyote yule kutoka kokote kule.Wanachosubiri sasa wao kama viongozi,kocha aseme anamtaka nani wamletee kwani pesa ipo.
Wakati huohuo Mkemi amesema kesho Jumapili Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kucheza na AFC bila ya wachezani wake wanne ambao wako kwenye majukumu ya timu zao za taifa.
Mkemi amewataja wachezaji hao kuwa ni Hassan Ramadhani Kessy,Beno Kakolanya,Mwinyi Hadji Mgwali na Mnyarwanda Haruna Hakizimana Niyonzima.
(KAGERA SUGAR)
Kocha Meck Maxime wa Kagera Sugar amefunguka Kuwa Kocha wa Yanga George Lwandamina ameonyesha nia ya Kufanya kazi naye, Haijaeleweka moja kwa moja kama atafanya naye kazi kama kocha msaidizi au atakuwa kwenye Benchi lake la Ufundi.
Maxime alisema
“Baada ya mechi yetu na Yanga ya msimu uliopita dhidi ya Yanga, kocha wao, Lwandamina alichukua mawasiliano yangu ambapo baadaye tulikutana na kuzungumza juu ya mambo mbalimbali lakini kubwa ni namna ya kujiunga na timu yao kwani anataka kufanya kazi na mimi.
“Licha ya kuongea huko, lakini mimi ni kocha siwezi kusema kwamba nitajiunga na timu fulani, lolote linaweza kutokea endapo tu tutakubaliana kwa vitu ambavyo nitakuwa navihitaji kwani huko nyuma nilishatoka Mtibwa na kwenda Kagera na hakutakuwa na maajabu kutoka hapa na kutua ndani ya timu hiyo,” alisema Maxime.
Facebook Comments
Share.

About Author