Home Michezo Top 10 ya wachezaji wenye ndege binafsi za ghali, CR7 kiboko

Top 10 ya wachezaji wenye ndege binafsi za ghali, CR7 kiboko

264
0

Orodha ya wachezaji wanaomiliko ndege za gharama duniani imetoka, kama ambavyo wengi walitarajia CR7 anaongoza orodha ya wachezaji wenye ndege za gharama kubwa duniani.

Cristiano Ronaldo. Cr 7 yuko juu kabisa katika orodha hii kwani achilia mbali na Ferrari na Galardo anazotumia bali Ronaldo ndio mwanasoka anamiliki ndege ya gharama duniani ni Gulfstream G650 inayouzwa £31.7m.

Lioneil Messi. Upinzani wa Cr7 na Lioneil Messi unaonekana sio uwanjani tu bali sasa hata nje ya uwanja kwani baada ya CR7 anayefuatia ni Lioneil Messi ambaye ana Embraer Legacy 650 yenye thamani ya £28.3m.

Zlatan Ibrahimovich. Kwa sasa ni majeruhi ndani ya Manchester United lakini maisha ya PSG, Barca, Intermilan na kwingineko yametosha kumfanya kuchuna mpunga wa kununulia  Citation Longitude yenye thamani ya £23.8m.

David Beckham. Bado yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaodaiwa kuweka pesa nyingi sana bani na Beckham kwake haikuwa shida kwenda kuitafuta Bombadier Challenger 350 iliyomgharimu 21.5m

Paul Pogba. Mchezaji ambaye amewahi kushikilia rekodi ya usajili ghali wakati akitoka Juve kwenda Manchester United, Gulfstream G280 ndio ndege anamiliki Pogba na ilimgharimu £20.4m.

Wayne Rooney. Aliuzwa na United kwenda Everton katika dirisha lililopita la usajili lakini kipesa bado yuko vizuri, Rooney anatumia Dassault Falcon 900LX ambayo thamani yake £15.8m.

Neymar. Kati ya wachezaji ambao wanapenda sana anasa ni Neymar, hakuwa anapewa pesa nyingi sana lakini kama kawaida ya Wabrazil hawana masihara yakija masuala ya matumizi, Neymar ana Embraer Legacy 450 ambayo thamani yake ni £12.2m.

Gareth Bale. Raia wa Wales huyu ambaye majeraha yamemfanya asifurahie soka siku za karibuni lakimi Bale anamiliki Cessna Citation XL Plus ambayo thamani yake ni £9.7m.

Kaka. Ricardo Kaka pamoja na kuwa mchezani anayelipwa sana lakini pia Kaka ni kati ya wanasoka ambao wanatokea kwenye maisha mazuri, Kaka ambaye kwa sasa amestaafu soka ana Cessna Citation Cj3 Plus ambayo thamani yake ni £6.4m.

Ronaldinho. Akiwa ametoka kutangaza kustaafu soka hivi majuzi tu lakini Gaucho yupo nafasi ya 10 katika wanasoka ambao wanamiliki ndege za gharama, Dinho ana Embraer Phenom ambayo aliinunua £2.9m.

CREDIT- shafii dauda

Leave a comment