Home News TRA yaelimisha wadau wa sekta ya kilimo Maonesho ya Nane Nane

TRA yaelimisha wadau wa sekta ya kilimo Maonesho ya Nane Nane

89
0
????????????????????????????????????

Na Mariam Mwayela- Nyakabindi-Simiyu
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya kodi katika sekta ya kilimo kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na vitongoji vyake pamoja na Mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro, Mbeya, Tabora na Lindi ambao wanatembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania katika Maonesho ya 25 ya Wakulima- Nane Nane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Akizungumza wakati wa Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Bw. Richard Kayombo, amesema kuwa Mamlaka kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Kilimo ina lengo la kutoa elimu ya Kodi katika sekta ya Kilimo kuhusu mambo mbalimbali wanayotakiwa kufanya katika biashara ya mazao pamoja na pembejeo za kilimo, kujasaji katika biashara zao pamoja na matumizi ya mashine za Kielektroniki za Kutolea risiti (EFD).

“Nawashauri wafanyabiashara na wananchi wa Mikoa ya Simiyu, Arusha, Mwanza, Morogoro, Mbeya, Tabora na Lindi kutumia fursa hii ya maonesho yaha kupata uelewa wa masuala ya kodi ili kufanya shughuli za kilimo katika mazingira mazuri”, alisema Kayombo.
Bw. Kayombo alisisitiza kuwa, kodi zinazolipwa zinasaidia kuboresha huduma za afya na miundombinu ambayo inasaidia wakulima kupeleka pembejeo shambani na kufikisha mazao ya kilimo sokoni kwa urahisi na kwa haraka bila usumbufu wowote.
Aliongeza kuwa Wafanyabiashara wote wa bidhaa za kilimo au pembejeo wenye mauzo kuanzia Milioni 14 na kuendelea anapaswa kuwa na mashine za kutolea risiti za kielektroniki na kutoa risiti kila anapofanya mauzo.

“Ni wajibu wa kila mfanyabiashara anayetakiwa kuwa na mashine za kutolea risiti za kielektroniki awe nazo na azitumie ipasavyo, mfanyabiashara yeyote ambaye hatatoa risiti za kielektroniki au kutoa risiti kwa udanaganyifu atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni fine ama kupelekwa mahakamani kwa Yule atakaye onekana anaendelea kukiuka sheria”, alisisitiza Kayombo

Bw. Kayombo alitoa wito kwa wananchi wote kudai risiti za kielektroniki pindi wanapofanya manunuzi kwani ni haki ya mwananchi kisheria na kutokufanya hivyo kunaweza kupelekea mwananchi kulipa faini kuanzia shilingi 30,000 hadi 1,500,000 kutokana na thamani ya mzigo.

 “Lengo la Mamlaka sio kutoa adhabu bali ni kuhakikisha kila mtu anafahamu wajibu wake na kujenga utamaduni mzuri wa kulipa kodi kwa hiyari ili kuongeza mapato ya Serikali”, aliongeza Kayombo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania inashiriki Maonesho ya Nane Nane ambayo yanafanyika Kitaifa katika Mkoa wa Simiyu pamoja na Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Morogoro, Arusha, Mbeya, Tabora na Lindi ambapo TRA inatoa huduma mbalimbali ikiwemo Elimu ya Kodi katika sekta ya kilimo, kodi mbalimbali, umuhimu wa kodi, pamoja na kutoa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi kwa wananchi wanaohitaji.

wanafunzi wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa tra