Uganda imeyaaga rasmi mashindano ya AFCON 2017 - The Choice

Uganda imeyaaga rasmi mashindano ya AFCON 2017

0

Uganda fans

Mabingwa wa kihistoria wa kombe la mataifa ya Afrika timu ya Misri, wameitupa Uganda nje ya michuano hiyo inayoendelea nchini Gabon baada ya kutandika bao 1-0 kwenye uwanja wa Port Gentil.

Baada ya kukaza kwa dakika 87, Uganda Cranes walishtukizwa na shuti la Abdallah El-Said dakika ya 88 bao ambalo lilipikwa na Muhammad Salah mshambuliaji wa Misri anayecheza klabu ya AS Roma ya Itania.

Kichapo hicho kwa Uganda kinamaanisha moja kwa moja hawana nafasi kusonga mbele kwenye michuano ya AFCON 2017 wakiwa wamesaliwa na mechi moja mkononi dhidi ya Mali.

Uganda walipoteza mechi yao ya kwanza ya Kundi D baada ya kufungwa 1-0 na Ghana ambao tayari wameshafuzu kucheza robo fainali kufatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Mali.

Kwa upande wa Misri, wao wanahitaji sare tu katika mchezo wao dhidi ya Ghana ili kufuzu hatua ya robo fainali bila kujali matokeo ya mechi kati ya Uganda vs Mali.

Share.

About Author