Uongozi Yanga Wamshitukia Donald Ngoma - The Choice

Uongozi Yanga Wamshitukia Donald Ngoma

0
Kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga na Simba, Athuman Idd ‘Chuji’ amekerwa na tabia ya Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma huku akimtuhumu kuwa ndiye anayefanya timu hiyo kuyumba katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.
Mshambuliaji huyo, hivi karibuni alitakiwa kupelekwa hospitali kwa ajili ya vipimo ili kujua kama amepona baada ya kuhisiwa kama anaudanganya uongozi wa timu hiyo kuwa ni mgonjwa.
Chuji alisema asingeweza kumvumilia mshambuliaji huyo akiwa nje ya uwanja akidanganya ana majeraha huku mwenendo wa timu yake ukiwa mbaya huku akiendelea kula mshahara wa bure.
“Niseme kuwa, siku zote ili ushindi upatikane ni lazima uwepo umoja na ushirikiano na kila mmoja kutimiza majukumu yake ya ndani ya uwanja katika kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa.
“Kiukweli, mimi kama ningekuwa Yanga hadi leo nikuhakikishie huyo Ngoma nisingeweza kumvumilia ningemtimua, yaani ni bora tukabaki wachache katika timu tungepambana wenyewe kuliko kubaki na mchezaji anayeturudisha nyuma.
“Angeondoka yeye, angekuja mchezaji mwingine mwenye uwezo mkubwa, wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo Ngoma wanayemnyenyekea,” alisema Chuji aliyeipandisha Coastal Union kucheza Ligi Kuu Bara

3,345 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author