USAIN BOLT KIBOKO ...HIVI NDIVYO ALIVYO IONGOZA JAMAIKA KUIBUKA KIDEDEA USIKU WA LEO - The Choice

USAIN BOLT KIBOKO …HIVI NDIVYO ALIVYO IONGOZA JAMAIKA KUIBUKA KIDEDEA USIKU WA LEO

0

Mwanariadha Usain Bolt ameiwezesha nchi yake ya Jamaica kushinda mbio za vijiti (4✖️100m Relay) katika usiku wa kuamkia leo kwenye michuano ya Olympics,Rio.

Bolt,29,akiwa na wenzake Nickel Ashmeade , Yohan Blake na Asafa Powell wameshinda mbio hizo wakitumia sekunde 37.27 na kuchukua medali ya dhahabu, Japan wakitumia Sekunde 37.60 na kuchukua medali ya Fedha huku Canada wakichukua medali ya shaba baada ya USA ambao walimaliza nafasi ya 3 kunyang’anywa ushindi kutokana na kufanya makosa katika kupokezana vijiti.

Usain ameweka rekodi ya kuwa mwanariadha wa kwanza na pekee kushinda medali 3 za dhahabu katika mbio za mita 100,200 na 4✖️100 Relay kwa mara 3 mfululizo katika michuano ya Olympic

Mjamaica huyo ameshinda mbio za mita 100,200, 4✖️100 Relay katika michuano ya Olympic 2008 Beijing,2012 London na 2016 Rio, Triple – Triple.
.
“Mimi ni bora zaidi,ninafuraha na ninajisifu mwenyewe , nimekamilisha malengo,nitakaa macho mpaka usiku mwingi ” amesema Bolt baada ya kushinda medali 9 za dhahabu za Olympic.
.
“Niliwaambia hawa wenzangu, kama hatutashinda hii, nitawapiga” amesema Bolt.

Medali 9 za dhahabu katika Olympics kwa mwanaridha huyo ni historia kubwa na hii inaweza kuwa ni michuano yake ya mwisho ya Olympic kushiriki.

#Rio2016

Share.

About Author