Home Michezo USAJILI YANGA: WAZIRI JUNIOR NA YANGA NDO IKO HIVI..

USAJILI YANGA: WAZIRI JUNIOR NA YANGA NDO IKO HIVI..

150
0
Waziri Junior baada ya kusaini Azam ameweka wazi kile kilichomkimbiza kuingia mkataba na mabingwa wa soka nchini Yanga na kutua Azam ambapo ametamka kwamba hawakuwa siriazi na maneno yalikuwa mengi kuliko vitendo ambavyo haviendani na hali halisi.
Waziri ambaye ametokea Toto African ya jijini Mwanza iliyoshuka daraja alisaini mkataba wa miaka miwili na Azam FC akitokea kuwasikiliza Yanga ambao alishawahakikishia kwamba wasiwe na wasiwasi.
“Yanga walikuwa wa kwanza kuzungumza nami, Azam wamefuata, nilikwenda pale Yanga kuzungumza nao lakini wanaonekana ni watu wenye maneno mengi, sielewi tatizo ni nini ndiyo maana niliona ni vyema niende Azam ambako pia walikuwa wanahitaji huduma yangu.
“Ni kweli Yanga wanashiriki mashindano makubwa lakini ushiriki wao kwangu haunisaidii kitu chochote naangalia maisha, kama kushiriki michuano mikubwa sioni maana kwani wanaenda na wanarudi bila faida, hivyo nimefanya uamuzi sahihi ambao nimeuamua mwenyewe bila kushinikizwa na mtu,” alisema Waziri Jr.