Ushindi wa Simba dhidi ya Majimaji umewasogeza kwa Yanga

0

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi leo kimeibuka na ushindi wa magoli 3-0 ugenini dhidi ya Majimaji FC kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Magoli ya Simba yamefungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 19 kipindi cha kwanza, dakika ya 63 Said Ndemla akafunga bao la pili na Laudit Mavugo akafunga goli la tatu dakika ya 89.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuifukuza Yanga kwa tofauti ya pointi moja baada ya kufikisha pointi 48 huku Yanga wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa pointi zao 49 baada ya timu zote mbili kucheza michezo 21.

Facebook Comments
Share.

About Author