VIDEO: Misri wamefuta ndoto za kocha wa Morocco kuweka rekodi Afrika - The Choice

VIDEO: Misri wamefuta ndoto za kocha wa Morocco kuweka rekodi Afrika

0
Misri imewatupa Morocco nje ya michuano ya Afrika kwa bao la Mahmoud Abdel-Moneim lililofungwa dakika ya 87 na kuwafanya Misri kuwa timu ya nne kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mwaka 2017.

Misri wakiwa ndiyo timu yenye mafanikio zaidi inapokuja suala la michuano ya Afrika wakiwa na historia ya kubeba taji hilo mara saba bado hawajafungwa goli hata moja tangu kuanza kwa michuano ya mwaka 2017 huko Gabon.
Misri itakutana na Burkina Faso ambao waliitoa Tunisia kwa ushindi wa magoli 2-0 kwenye mchezo wao wa robo fainali siku ya Jumamosi.
Kuondolewa kwa Morocco kwenye mashindano kuna zima ndoto za boss wa timu hiyo Herve Renard kutwaa taji la Afrika mara tatu akiwa na timu tofauti.

Mfaransa huyu aliiongoza Zambia kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2012 na mwaka 2015 akashinda taji hilo akiwa na Ivory Coast.

Share.

About Author