Wachezaji 10 waliofeli baada ya kusajiliwa na Manchester United. - The Choice

Wachezaji 10 waliofeli baada ya kusajiliwa na Manchester United.

0

fdfsd

Memphis Depay anakaribia kujiunga na Olympique Lyon ya Ufaransa.Depay kabla ya kujiunga na United alikuwa mfungaji katika ligi ya Uholanzi.Uwezo wake ndani ya uwanja ulionekana kuwa mkubwa sana hasa kipindi cha kombe la dunia lililofanyika Brazil.Depay ujio wake United ulikuwa na matarajio makubwa,mashabiki wengi wa United waliamini ni Cristiano mpya amekuja.

Chini ya Van Gaal Depay hakuonesha makali yake na baada ya kuja kwa Mourinho pia ameshindwa kumshawishi kupata namba katika kikosi chake.Jose ameamua kumuacha aondoke,lakini unadhani Depay ndiye mchezaji wa kwanza kuja United na kuwa tofauti na matarajio ya mashabiki?Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wengine waliokuja United kwa matarajio makubwa wakaboronga.

1.Radamel Falcao.Alikuja United kwa mkopo lakini mkopo huo uliwagharimu United £16m kwan kila mwisho wa wiki Falcao aliweka £260 000 mfukoni.Akiwa kati ya wachezaji wanaojua kucheka na nyavu,Falcao alifunga magoli manne tu katika mechi 29 alizovaa jezi ya Man United.Pia alikua na majeruhi ya mara kwa mara baada ya hapo United alienda Chelsea nako akiboronga ila sasa karudi Monaco na kugeuka lulu,katika mechi 14 alizocheza Ligue 1 Falcao amefunga magoli 11.

2.Angel Di Maria.Ilikuwa mwezi wa nane mwaka 2014 Manchester United wakatoa kiasi cha £59m kumnunua mshambuliaji huyo wa Argentina.Kila timu pinzani ilishikwa na hofu kuhusu ujio huu kwa kuwa uwezo wa Di Maria ulikuwa mkubwa sana.Di Maria aliboronga United lakini pia nje ya uwanja matukio ya familia yake kuvamiwa pia alianza kuwa na tofauti na kocha mkuu Van Gaal.Baada ya msimu mmoja aliondoka alipohojiwa miaka miwili baadae na jarida la michezo liitwalo L’Equipe Di Maria alisema “kilichontokea United kinahuzunisha na sitaki kukumbuka maisha ya pale”.

3.Memphis Depay.Aliitwa Ronaldo mpya na ili kuonesha kumuamini alipewa jezi namba 7 jezi ambayo huvaliwa na wachezaji manguli.Depay baada ya muda alianza kuonekana akiboronga.Mashabiki wengine wakimuona mvivu huku wengine wakisema ni bishoo sana.Alishindwa kuwapa United kile walichotaraji huku msimu huu Mourinho akimpa nafasi mara nne tu na kisha kuachana nae.

4.Massimo Taibi.Hili linaweza kuwa jina geni kwa mashabiki vijana wa Manchester United.Baada ya Peter Schmeicles kuonekana anataka kuacha kucheza soka,mwaka 1999 United waliamua kutafuta mbadala wa kipa huyo.United waliilipa £4.5m kumpata Mataibi.Kilichotokea baada ya Mataibi kukaa golini ilikuwa ni kilio kwani katika mechi 4 za mwanzo alifungwa goli 11.Mabosi wa United hwakuweza kumvumilia kwani mwaka 2000 tu walimuondoa klabuni hapo.

5.Sebastian Veron.Alisajiliwa kwa £28.1 na kuaminika sana kwani kocha Alex Ferguson alisema Veron ni kati ya world class player wanaokuja United kufanya kazi.Veron hakuonekana na thamani aliyosajiliwa United,katika mechi 81 alifunga goli 11,baada ya United kutoridhishwa na kiwango chake waliamua kumuuza Chelsea kwa bei ya hasara ya £15m.

6.Kleberson.Mwaka 2003 mwezi wa nane United walimsajili Kleberson.Akiwasili siku moja na Cristiank Ronaldo walitarajiwa wawili hao kufanya makubwa katika ligi ya Uingereza.Kleberson alisajiliwa kuchukua nafasi ya Sebastian Veron.Tofauti na mwenzie Crstiano Ronaldo,Kleberson alikua mbovu sana.Katika mechi 30 akiwa na United alifunga magoli mawili tu.

7.Bebe.Hadi leo wachambuzi wanajiuliza Ferguson alimnunuaje Bebe?Ferguson alikiri kutowahi kumuona Bebe akicheza hapo mwanzo,lakini aliwagharimu £7.4m akiwa klabuni hapo.Usajili huu ulitokana na shinikizo la aliyekuwa kocha wa Man United Carlos Queiroz,kutokana na kuwa na uwezo mdogo United walimpa nafasi mara 7 tu na akafunga goli 1,sasa yuko Eibar Hispania.

8.Wilfred Zaha.Aliichezea England na sasa karudi nyumbani kwa wazazi wake Ivory Coast na yupo kwenye Afcon.Mbio zake na uwezo wa kudrible naye pia walisema ni Ronaldo mpya.Ferguson wakati anaondoka United alimuacha Zaha katika mikono ya moyes ambae hakuwa na imani naye mdani na nje ya uwanja.Zaha inasemekana alikuwa na tofauti na Moyes kuanzia nje ya uwanja baada ya Van Gaal kuja na Depay pamoja na Di Maria aliamua kumuacha Zaha aondoke na sasa yupo Crystal Palace.

9.Eric Djemba Djemba.Mcameroon huyu alisajiliwa kwa dau la £3.5m.Eric aliaminika atakuja kuwa Roy Keane mpya United lakini mhh.Hakuwa na kiwango kizuri hata kidogo na alishindwa kumshawishi Ferguson.Alicheza mechi 39 tu na kupata magoli mawili baada ya miezi 18 United walimuondoa.

10.Zoran Tosi.Mwaka 2009 winga huyu alionekana kama Giggs.Mabosi wa Manchester wakaona isiwe tabu wanamuhitaji Giggs mpya.Waliingia mfukoni wakatoa kiasi cha £7m kumnunua winga huyo.Alipata nafasi kucheza United mara tano tu huku akiondoka bila goli baadae iuzwa CSKA Moscow.

Share.

About Author