Home Michezo WACHEZAJI HAWA 12 KUPIGWA PANGA YANGA BAADA YA MSIMU KUISHA

WACHEZAJI HAWA 12 KUPIGWA PANGA YANGA BAADA YA MSIMU KUISHA

233
0

Wachezaji hawa 12 Kupigwa panga Yanga baada ya Msimu kumalizika

Katika hali inayoonekana ni ya kuondoa wachezaji ambao msaada wao umepungua kwenye timu Kuna habari za ndani kuwa klabu ya Yanga Ipo katika mchakato wa kuwatema wachezaji 12 mara tu baada ya kumalizika kwa msimu wa mwaka 2017/2018.

Baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kukumbumbana na Panga hilo ni Geofrey Mwashiuya, Amis Tambwe, Donald Ngoma, Pato Ngonyani, Fiston Kayembe ambaye usajili wake umeingia Doa na Kuyshindwa kuitumikia Yanga mpaka sasa.

Wengine   ni Nahodha wao Mkongwe Nadir Haroub Cannavaro ikielezwa sababu ya Umri na uwezo wake Kushuka, Beno Kakolanya wengine ni  Said Mussa, Yusuph Mhilu, na Edward Maka hawa wakitokea Yanga B.

Wachezaji hao inaelezwa kuwa wamekuwa na mchango mdogo ndani ya Kikosi cha Yanga ndani ya Msimu Huu huku baadhi yao wakiwa na majeraha yanayoonekana kuwa ya mrefu, hata hivyo mtu wa Mwisho kuamua inaelezwa itakuwa ni ripoti ya Mwalimu George Lwandamina