Home News WANAHABARI NA WATAALAM WA HALI YA HEWA WAKAA MEZA MOJA KUJADILI UTABIRI...

WANAHABARI NA WATAALAM WA HALI YA HEWA WAKAA MEZA MOJA KUJADILI UTABIRI WA MVUA ZA MASIKA

805
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang’a akifungua warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). 
Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri – TMA, Bw. Samwel Mbuya akiwasilisha mada katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 
Mtaalamu (Utabiri) wa Hali ya Hewa, Elias Lipiki akiwasilisha mada kwa wanahabari katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 
Mwanahabari Faustin Shija kutoka Nipashe, akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA. 
Jerome Mshanga wa Clouds Media akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA kwenye warsha hiyo. 
Mwanahabari na Bloga, John Bukuku akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang’a akifafanua jambo kwenye warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).(PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG)
                         XXXXXXXXXXXXXXX

Washiriki wa warsha ya wanahabari kuhusu msimu wa mvua za masika, mwezi Machi hadi Mei 2019 katika picha ya pamoja

Tarehe 13 Februari 2019
Ikiwa ni mwendelezo wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua za MASIKA kwa 2019 kabla ya kutolewa rasmi kwa umma tarehe 14 Februari 2019.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa ‘Law School’, Dkt. Ladislaus Changa ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya tarifa za hali ya hewa wa TMA alisema kuwa dhamira ya kukutana na wanahabari ni muendelezo wa dhamira na utaratibu wa TMA wa kuimarisha ushilikishwaji na kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari ili wazielewe vizuri zaidi taaarifa za hali ya hewa na hususan utabiri na hivyo waweze kuzifikisha tarifa, kuhabarisha na kuelimisha jamii kwa ufasaha na ufanisi zaidi.

Aidha wanahabari walitumia fursa hiyo kujadili na kutoa mapendekezo ya kuboresha ufungashwaji na usambazaji wa tarifa za hali ya hewa ili ziendelee kuwafikia walengwa kwa wakati na kwa ufasaha zaidi. Pia walielezea umuhimu wa kuwajengea uwezo wanahabari kuzielewa kwa kina tarifa za hali ya hewa na mabadiliko yake.

Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa chini ya mwamvuli wa Awamu ya Pili ya Programu ya Kidunia ya Utoaji wa Huduma za Hali ya Hewa ya GFCS yaani “Global Framework for Climate Services Adaptation Programme in Africa (APA) II” hapa Tanzania yenye lengo la kuimarisha huduma za hali ya hewa katika nyanja ya utoaji, usamabazaji na utumiaji wa huduma hizo. Mkutano huu ulijumuisha wanahabari kutoka kwenye vituo vya televisheni, redio, magazeti, blogs na mitandao ya kijamii

IMETOLEWA NA
OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
1