Home News WATAALAMU WA CHUMBA CHA UPASUAJI MOI,MNH WABADILISHANA UZOEFU

WATAALAMU WA CHUMBA CHA UPASUAJI MOI,MNH WABADILISHANA UZOEFU

848
0

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Muhimbili bwana Yasini Munguatosha akizunguumza jambo katika kikao hicho.

Wataalamu wa chumba cha upasuaji kutoka MOI na MNH wakifuatilia jambo

Mkurugenzi wa Hudum za Uuguzi MOI akimkabidhi keki Mkurugenzi wa Uuguzi Muhimbili ,keki hiyo imetolewa kama ishara ya kudumisha ushirikiano kati ya hospitali hizi Mbili, nyuma ni watumishi katika chumba cha upasuaji MOI na Muhimbili
…………………………………..
Dar es Salaam, 17/10/2018.Timu ya wataalamu wa chumba cha upasuaji ya Taasisi ya Mifupa MOI leo imekutana na kufanya majadiliano na timu ya chumba cha upasuaji ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kupeana mbinu za kimkakati za kuboresha huduma na kubadilishana uzoefu ili kuendelea kuboresha huduma za upasuaji katika hospitali zote mbili.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi mdogo uliopo katika chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo timu ya MOI ilikongozwa na Mkurugenzi wa huduma za uuguzi bwana Fidelis Minja na timu ya Muhimbili ikiongozwa na bwana Yasini Munguatosha .

Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi MOI bwana Fidelis Minja amesema Taasisi ya MOI inaushukuru uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ushirikiano ambao umekuwepo kati ya hospitali hizi mbili jambo ambalo limepelekea hali ya utoaji huduma kuwa bora kwa wagonjwa.

“Kwa niaba ya Bodi ya wadhamini, Mkurugenzi mtendaji na jumuiya nzima ya MOI tunawashukuru sana uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa ushirikiano mkubwa ambao tumekuwa tukipata hapa, miezi michache iliyopita tulipata chnagamoto kwenye Mitambo yetu  ya vyumba vya upasuaji jambo ambalo lilipelekea baadhi ya vyumba kufanyiwa matengenezo, tunashukuru tulipata vyumba vya upasuaji hapa na huduma ziliendelea kama kawaida na hapakuwa na malalamiko yoyote” alisema Bwana Minja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bwana Yasini Munguatosha amesema ni heshima kubwa kupata ugeni ambao umelenga kubadilishana uzoefu na kuboresha huduma kwa watanznia na pia shukrani zenye lengo la kuudumisha udugu kati ya Taasisi hizi mbili uliodumu kwa miaka mingi.

“ Nilivyosikikia kuna ujio wa ndugu zetu wa MOI nilifarijika sana maana hospitali zetu hizi zina historia ndefu sana ambayo wengine tumeikuta na ni budi tuiendeleze, Muhimbili pia imekuwa ikipata ushirikiano mkubwa kutoka MOI, kuna kipindi oparesheni za Muhimbili za meno, masikio ,pua , koo na za Moyo zilikua zinafanyika MOI hivyo ni vyema tukaendelea kushirikiana pale panapokuwa na changamoto lengo ikiwa ni huduma bora kwa watanzania wenzetu”. Alisema Bwana Munguatosha

Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa vitengo vya usingizi vya MOI na Muhimbili, wakuu wa chumba cha upasuaji MOI na Muhimbili pamoja wa wahudumu wa vyumba vya upasuaji vya hospitali zote mbili ambao kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza ushirikiano huo kati ya Hospitali hizi mbili ambazo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa Tanzania na nchi nyingi za ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.