Home Michezo Watatu Simba waliokubali kutolewa kwa Mkopo hawa hapa

Watatu Simba waliokubali kutolewa kwa Mkopo hawa hapa

1383
0

Watatu Simba waliokubali kutolewa kwa Mkopo hawa hapa

November 15 2018 Dirisha dogo la usajili litafunguliwa rasmi huku timu mbalimbali zikiwa zimejipanga kuboresha vikosi vyao kwaajili ya kuhakikisha zinafanya vyema.

Moja kati ya timu ambayo inaelezwa kuwa katika mikakati ya Kupunguza na Kuongeza nyota wao ni mabingwa wa soka nchini Tanzania klabu ya Simba.

Simba inaelezwa kuwa katika mipango ya kuwatoa kwa mkopo baadhi ya nyota wake ambao wako vizuri lakini wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza.

Mpaka sasa taarifa za uhakika ambazo kwata Unit app imezipata ni kwamba Wachezaji Said Mohammed Nduda, Marcel Kaheza na Mohammed Rashid “T-Better” wamekubali kutolewa kwa mkopo lakini kwa sharti la kuwa wanapewa nafasi ya kucheza katika timu watakazokwenda