Home News WAZIRI KALEMANI AIPONGEZA TANESCO, MIKAKATI MIPYA YAWEKWA KUFIKISHA UMEME NCHI NZIMA

WAZIRI KALEMANI AIPONGEZA TANESCO, MIKAKATI MIPYA YAWEKWA KUFIKISHA UMEME NCHI NZIMA

69
0

Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI akizungumza Dodoma katika kikao kazi alichofanya na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini Dkt TITO MWINUKA (Kulia) akifuatilia kwa Makini Mkutano wa Kikao Kazi Ulioitishwa Mjini Dodoma na Waziri wa Nishati Dkt KALEMANI na Kuhudhuriwa na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA.

Watumishi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, akiwemo Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Bi Leila Muhaji wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI alipokuwa akizungumza Kwenye Kikao Kazi aliouitisha Mjini Dodoma na Kuhudhuriwa na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA.

Wajumbe wa Bodi ya Tanesco, Viongozi wa Menejimenti ya Tanesco, Bodi ya EWURA na Watendaji wa REA Wakiwa Kwenye Kikao Kazi Kilichoitishwa na Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI Mjini Dodoma.

Waziri wa Nishati dkt.medard matogolo kalemani amelipongeza shirika la Umeme  Tanzania Tanesco  kwajitihada wanazozifanya kwani sasa hali ya umeme imetengemaa ukilinganisha na siku za nyuma kuanzia miez ya septemba mpaka Machi mwaka huu.
Waziri aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, mjini Dodoma katika kikao kazi alichofanya na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wamenejment TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA
Kwanza nianze kwa Kumpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, na Wajumbe wote wa Bodi pamoja na menejment yote ya TANESCO ikiongozwa na Mkurugenzi wao Dkt. Tito E. Mwinuka   kwa kazi nzuri wanayoifanya , sasa ivi hali ya Umeme imeimarika,na taarifa za mrejesho tunazozipata kutoka wateja ni kuwa hali ya Umeme inaridhisha kwa sasa tofauti na kipindi cha nyuma , niwapongeze mameneja wote wa mikoa na Kanda  wanafanya kazi nzuri hasa upande  wa Uzalishaji wa Umeme na Usafirishaji wa Umeme.
Aidha Waziri kalemani amesema kuwa lengo kubwa la kukutana na viongozi wote wa TANESCO, REA na EWURA ni kujiwekea mikakati yakuhakikisha malengo yanatimiwa,changamoto zinatatuliwa na kuhakikisha miradi ya REA  awamu ya Tatu inatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati, kwani  Nishati ndio msingi mkuu wa Maendeleo ya Viwanda na hivyo sasa Serikali haitovumilia uzembe wowote utakao jitokeza ambao utarudisha nyuma miradi ya REA.
“Mameneja wote wa Mikoa na Kanda wahakikishe  watu wanawekewa umeme kwa wakati, na maagizo ya kuhakikisha vijiji 3  kwa wiki vinawekewa Umeme, wahandisi wote waliopewa kazi hizo wahakikishe zinafanyika na vinginevyo wakae pembeni, Meneja ukiona mhandisi husika anashindwa  muweke pembeni, mtafutie kazi ya kufanya  na Mkandarasi anaeshindwa kukamilisha kazi kwa wakati achukuliwe hatua” .
Nae Meneja wa Kanda ya kati TANESCO mhandisi Atanasius Nangali amesema kuwa TANESCO kanda ya kati imejipanga vizuri katika  kuhakikisha  agizo la muheshimiwa waziri linatekelezwa.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na viongozo mbalimbali akiwemo Naibu waziri wa Nishati mheshimiwa Subira mgalu,na makamishna wa Wizara .