Home News WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA USHIRIKA KUTOONDOLEWA ENEO LA LAMBO ESTATE...

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA USHIRIKA KUTOONDOLEWA ENEO LA LAMBO ESTATE NA KUPATIWA EKARI MBILI KILA MMOJA

1021
0

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro.

Baadhi ya wananchi wa eneo la Shamba la Lambo Estate katika wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro wakifurahia baada ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa maagizo wananchi hao wasiondoke katika eneo hilo sambamba na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.

Baadhi ya wananchi wa eneo la Shamba la Lambo Estate katika wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro wakifurahia baada ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa maagizo wananchi hao wasiondoke katika eneo hilo sambamba na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipata maelezo ya mashine iliyotengenezwa katika  Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai kutoka kwa meneja wa kiwanda hicho Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro.

 

Baadhi ya nyumba za wananchi waliokuwa wafanyakazi wa Ushirika katika eneo  la Lambo Estates wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambao Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi aliamuru wasiondoke eneo hilo na kuwapatia kila mmoja ekari mbili kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao ikiwa ni utatuzi wa mgogoro wa muda mrefu
PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
……………………..
Na Munir Shemweta, WANMM Kilimanjaro
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekata mzizi wa fitna ambapo ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa chama cha ushirika katika eneo la Lambo Estate Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro kutoondolewa katika eneo hilo na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaisha.
 
Uamuzi  huo wa Lukuvi wa kutoa ekari mbili kwa wananchi hao 78 unafanya kutolewa kwa jumla ya ekari 156  kati ya ekari 1600 . Uamuzi huo unafuatia mgogoro wa muda mrefu baina ya waliokuwa wafanyakazi wa ushirika na uongozi .Mgogoro huo umeibuka baada ya wafanyakazi hao kutakiwa kuondoka katika makazi yaliyopo kwenye eneo la shamba  kutokana na utumishi wao kukoma.
 
Waziri Lukuvi alitoa maamuzi hayo leo katika wilaya Hai  ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kutembelea wilaya za Hai, Moshi na Same kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya hizo mkoa wa Kilimanjaro.
 
Mhe Lukuvi ameshangazwa na ushirika wa watu wachache kutaifisha ardhi na kuamuru watu waliokuwepo muda mrefu katika eneo la lambo estate kuondoka na kusema kuwa safari hii serikali itawanyoosha wale wote wanaofanya ujanja wa kuwaonea wanyonge.
 
*”Sijawahi kuona ushirika wa namna hii ambapo wenye rasilimali hawanufaiki na ardhi iliyopo katika  kijiji chao halafu ardhi hiyo inakodishwa kwa wanachama wa ushirika wanaotoka  vijiji vingine”*  alisema Waziri Lukuvi.
 
Huku akishangiliwa na wananchi wakati akitoa maamuzi hayo, Mhe. Lukuvi alisema  amekwenda katika eneo hilo la Lambo Estate kushughulikia mgogoro wa ardhi. Suala la ushirika litashughulikiwa na waziri mwenye dhamana na vyama vya  ushirika ambae ataamua iwapo ushirika huo unafaa. Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa, serikali haiwezi kuwaondoa wazee  walioishi kwa muda mrefu.
 
Waziri wa Ardhi ametoa maagizo kwa wananchi watakaopewa ekari mbili kuwa maeneo watakayopatiwa ni kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na hawaruhusiwi kuuza na kwa yeyote atakayeamua kuondoka eneo hilo basi eneo hilo litabaki kuwa la serikali.
 
Kufuatia maelekezo hayo Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuanza mara moja zoezi la kuwagawia  wananchi ekari hizo kama ilivyoagizwa na  mhe Lukuvi.
 
Awali Katibu wa jumuiya ya wanaushirika Edward Chedi alimueleza Mhe Waziri Lukuvi kuwa mgogoro wa eneo hilo ulianza mara baada ya shamba hilo kutaifishwa na ajira za walikuwa wafanyakazi wa ushirika kukoma mwaka 2001 na kuwepo mfululizo wa kesi uliofikia ngazi ya Mahakama Kuu na kuagizwa waliokuwa wafanyakazi kulipwa mafao na kukabidhiwa vyeti vya kutambuliwa pamoja na ekari hamsini za kujikimu kwa kipindi  watakachokaa hapo kabla ya kuondolewa.