Home News WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA

1078
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi 
wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa Tanzania  katika Maadhimisho ya Siku
ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini 
Dar es salaam, Oktoba 24, 2018.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo Tanzania imeungana na nchi 189 duniani kwenye sherehe hiyo yenye kauli mbiu isemayo Uwezeshaji wa vijana kiubunifu kwa malengo ya dunia ya maendeleo endelevu.

Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa malengo ya maendeleo endelevu ya kidunia yanatimia ikiwemo upatikanaji wa elimu, Afya na ajira kupitia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini kupitia wizara husika.

Sambamba na hayo Waziri Majaliwa alisema kuwa Tanzania wanajali haki za wakimbizi waliopo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwarudisha nchi kwao pindi amani inapotengamaa kwa kujali utu na usalama wao.

“Tunajali utu na usalama wa wakimbizi waliopo hapa nchini ndio maana mpaka sasa zaidi ya wakimbizi elfu hamsini na mbili wamerudi nchini kwao ikiwa ni kati ya wakimbizi zaidi ya elfu themanini na moja waliopo hapa nchini.” alisema Majaliwa.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya (UN) nchini Alvaro Rodriguez amesemakuwa wakati wakiadhimisha miaka 73 toka kuanzishwa kwa shirika hilo wameweza kuwafikia watu mbalimbali wenye uhitaji pamoja na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo ameongeza kuwa katika sekta ya elimu wamesaidia upatikanaji wa huduma ya maji salama na usafi katika mshule 49 zenye jumla ya wanafunzu zaidi ya elfu ishirini na sita wengi wao wakiwa ni wasichana.

Katika hatua nyingine Waziri Majaliwa alisema kwamba nchini Tanzania hakuna ubanaji wa uhuru wa vyombo vya habari wala taasisi zisizo za kiserikali.

Alisema jambo hilo linadhihirishwa na uwepo wa jumla ya vituo vya redio 152, ambavyo kati yake ni vituo vitatu tu ndivyo vinavyomilikiwa na Serikali.

“Tunapenda kuwahakikishia kuwa, Serikali ya Tanzania inaongozwa na katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa kujieleza na kupata habari,” alisisitiza.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba mwananchi yeyote atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Alieleza kuwa Serikali imeridhia mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na ule wa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Sambamba na kusimamia haki hizo, Serikali imeendelea kutekeleza wajibu wake katika kuiwezesha jamii kuishi salama kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.

Alisema kukuza, kuimarisha na kulinda haki za binadamu ni wajibu wa Serikali na kwa kuzingatia umuhimu huo mwaka 1984 iliingiza sheria ya haki za binadamu katika katiba.