Waziri Mwakyembe Azishukia Simba na Yanga….”Hawako Series”

0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezishukia klabu za Simba na Yanga na kuzitupia lawama kuwa zimekosa nafasi muhimu ya kucheza na timu kubwa ya Everton ambayo jana imeshuka dimbani na klabu ya Gor Mahia

Katika mchezo wa jana ambao Everton waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki umempelekea Waziri Mwakyembe kutoa yake ya moyoni kwa klabu za Tanzania.

“Kwanza nafikiri hili liwe fundisho kwa klabu zetu za nyumbani mimi nina uhakika wanaweza kunisahihisha tulipowaambia kutakuwa na mashindano na timu ya Everton hapa kwa timu itakayoshinda sidhani kama walituamini, sababu timu walizokuwa wanaleta mlikuwa mnaziona wachezaji wale mahiri wengi walikuwa hawapo, mimi nilisikitika sana na niwe mkweli nilitamani sana timu ya Tanzania ndiyo icheze na Everton katika mchezo ule kwenye uwanja wetu ambao tumeuhangaikia sana kuweka nyasi mpya za muda” alisema Mwakyembe

Mbali na hilo Waziri Mwakyembe alitoa wito kwa klabu za Tanzania
“Jamani pale tunapowaambia kuna mashindano tuchukulie jambo hilo umuhimu, maana ujio wa Everton unafaidia kubwa tatu kwa taifa letu na Afrika Mashariki kiujumla moja ni kwa timu yenyewe ambayo imecheza nayo Gor Mahia pamoja na kufungwa lakini waliibuka mashujaa, kwa sababu wamepata uzoefu wa kimataifa na wameonekana dunia nzima, hivyo vijana wa Gor Mahia waliocheza vizuri kesho na kesho kutwa watatafutwa na watu wanaotafuta wachezaji, lakini pia imefunguka njia kwa dunia kwamba Tanzania ni nchi inayopenda michezo lakini imeonyesha kuwa tuna viwanja vya kimataifa hapa. Faida nyingine ni utalii imefungua njia kwamba Tanzania tuna vivutio vingi vya utalii” alisema Mwakyembe

Mbali na hilo Mwakyembe alisema kuwa timu ya Gor Mahia kucheza na Everton imewajengea kujiamini kwamba hakuna timu wanaweza kukutana nayo Afrika Mashariki ikawasumbua, na kudai kutokana na hali hiyo saizi timu yoyote itakayokutana na Gor Mahia itafungwa tu.

Facebook Comments
Share.

About Author