Waziri Mwijage awatangazia vita watumishi wa umma - The Choice

Waziri Mwijage awatangazia vita watumishi wa umma

0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametangaza vita kwa watumishi wanaoruhusu uingizwaji wa bidhaa bandia nchini, na kutoa onyo kwamba watakao fanya hivyo wajiandae kuondoka.
Mwijage ametoa onyo hilo juzi Bungeni mjini Dodoma, wakati akisoma bajeti ya wizara yake, ambapo pia alipiga marufuku bidhaa bandia kuingia nchini kutoka nje ya nchi kuanzia Julai mosi mwaka huu.
“Ikifika mwezi Julai mwaka huu, kama bidhaa feki zikipita kuingia nchini mtakuwa hamnitakii mema, na walio chini yangu mkae kabisa mkao wa kuondoka kama bidhaa zisizokidhi viwango zitapia na kuja kuumiza viwanda vyetu nchini,” alisema.
Facebook Comments
Share.

About Author