Home News WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA HALMASHAURI YA MADABA

WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA HALMASHAURI YA MADABA

1360
0

Mhandisi wa Wilaya ya Madaba, Jonas Maganga akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa chanzo cha Mradi wa Maji wa Maweso, mkoani Ruvuma.

Afisa Maji wa Bonde la Ziwa Nyasa, Mhandisi Elise Englebert akitoa taarifa kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa ofisi ndogo za Bonde la Ziwa Nyasa na Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini, Songea Mjini.

Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa (aliyevaa kofia) akiwa na viongozi wa Halmashauri ya Madaba akisikiliza taarifa kuhusu Mradi wa Maji wa Lilondo akiwa juu ya tenki la mradi huo uliopo wilayani Madaba, mkoani Ruvuma.

Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa akipita kukagua maendeleo ya ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Madaba, mkoani Ruvuma.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Madaba, mkoani Ruvuma.
…………………………..
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kukagua miradi ya maji ya Madaba, Lilondo na Maweso.
Miradi hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea inalenga kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji kwa maeneo ya vijiji hivyo, mkoani Ruvuma.
Akizungumza na wananchi wa Lilondo, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amepongeza juhudi za wakazi wa kijiji hicho wa kukabiliana na tatizo la maji kwa kujenga tenki la maji na kuahidi wizara yake itatoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mabmba na kazi ya ulazaji wa mabomba hayo kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi.
Amesema wananchi hao ni mfano wa kuigwa na kuwashukuru kwa nia yao njema ya kuinga Serikali mkono katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Maji.
Akitoa ahadi kwa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa atalipa fedha zilizobaki kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Lilondo na Maweso ili waweze kumaliza kazi ya ujenzi.
Aidha, Profesa Mbarawa ameanzisha zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji Maweso na kuitaka Serikali ya Kijiji na wananchi wapande miti ya kutosha na zoezi hilo liwe endeevu kwa lengo la kuwa na chanzo cha uhakika cha maji kwa miaka mingi.
Mradi wa maji wa mtiririko wa Lilondo umefikia asilimia 65 ya ujenzi, lengo la mradi likwa ni kutoa huduma kwa wakazi 5,919 ifikapo 2024 katika Kijiji cha Lilondo, utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1.048.
Huku mradi wa maji wa mtiririko wa Maweso ukiwa umefikia asilimia 65 ya ujenzi, lengo la mradi ni kutoa huduma ya maji kwa wakazi 2,876 ifikapo 2023 katika Kijiji cha Maweso, utagharimu zaidi ya Silingi Milioni 546.
Profesa Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku 6 mkoani Ruvuma ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji.