Web ametaja mchezaji na kocha aliyempa wakati mgumu enzi zake akichezesha soka - The Choice

Web ametaja mchezaji na kocha aliyempa wakati mgumu enzi zake akichezesha soka

0

1Refarii wa mstaafu wa England Howard Webb amesema David Moyed ni moja ya makocha waliokuwa wakimpa wakati mgumu sana pindi alipokuwa akichezesha mchezo unaohusu timu yake.

Akiwa amechezesha michezo mingi iliyokuwa ikizikutanisha timu za Everton na Manchester United, Webb alipata wakati mgumu sana kwenye michezo hiyo kutokana na upinzani wa makocha hao.

Akiongea na Daily Mirror Webb amesema: “Mtu ambaye alikuwa akiniumiza kichwa na ambaye alinifanya niichukuie taaluma ya urefarii, alikuwa David Moyes. Alikuwa mwepesi sana kunikosoa.”

Refarii huyo ambaye katika maisha yake ya kazi amechezesha karibu michezo 1,000 kabla ya kustaafu mwaka 2014, pia amesema kwamba Everton na Stoke City yalikuwa maeno magumu sana kwa maana ya kuexperience mazingira yasiyo rafiki.

Webb pia hakuishia hapo baada ya kuulizwa ni mchezaji gani ambaye alikuwa akimpa wakati mgumu kwenye kutoa maamuzi uwanjani.

“Craig Bellamy ni mchezaji niliyekuwa napata wakati mgumu sana lnapokuja suala la kukabiliana naye, alikuwa ni mwepesi kutoa maoni yake na kutokupa nafasi ya kukusikiliza.”

Facebook Comments
Share.

About Author