Home Michezo YANGA 0-0 TUSKER (4-2) ‘LIVE’ FULL TIME, SPORTPESA SUPER CUP, UWANJA WA...

YANGA 0-0 TUSKER (4-2) ‘LIVE’ FULL TIME, SPORTPESA SUPER CUP, UWANJA WA UHURU

207
0

FULL TIME

Yanga wanasonga mbele kwa penalti 4-2 baada ya wachezaji wawili wa Tusker kukosa penalti.

Yanga 

Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anapata

Obrey Chirwa anapata

Maka anapata

Said Musa anapata

Tusker 

Isike anapatapa

Brian anapata

…..Anakosa

Ousu anakosa

Sasa ni muda wa kupigiana penalti.

Dakika 90 zimekamilika, mwamuzi anazungumza na manahodha kwa ajili ya kujiandaa kwenda kupiga penalti.

Mwamuzi anamaliza mchezo.

Dakika ya 90: Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Bakary Osman anatoka Yusuph Mhilu.

Dakika ya 89: Yanga wanafanya shambulizi kali lakini kipa wa Tusker anakuwa makini.

Dakika ya 88: Tusker wanaonyesha kujiamini.

Dakika ya 87: Kasi ya mchezo siyo kubwa na timu sasa zinacheza kwa umakini mkubwa.

Dakika ya 85: Tusker wanafanya shambulizi kali langoni mwa Yanga, inaokolewa na kuwa kona, inapigwa kona lakini inakosa mmaliziaji.

Dakika ya 82: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Juma Mahadhio anaingia Samuel Greyson.

Dakika ya 80: Alan Wanga wa Susker anafika langoni mwa Yanga lakini beki Vicent Andrew anafanya kazi nzuri.

Mashabiki wa Yanga wanamshangilia Said Musa ambaye anakuwa na kasi kila anapopata mpira.

Dakika ya 74: Mchezo ni mgumu, kasi imepungua kwa timu zote kucheza kwa kuonekana kuwa makini.

Dakika ya 70: Yanga wanapata nafasi mbili za kufunga lakini washambuliaji wakosa umakini. Yanga wanaonekana kutafuta bao kwa nguvu.

Dakika ya 65: Upinzani ni mkali na mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 61: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Emanuele Martine anaingia Said Musa.

Kumbuka Yanga leo ipo chini ya Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi.

Dakika ya 55: Mchezo ni mgumu kwa timu zote kila upande unaonekana kuwa vizuri.

Dakika ya 50: Yanga wanajibu mapigo kw akupiga pasi lakini bado Tusker ndiyo ambao wameendelea kutawala mchezo.

Dakika ya 48: Susker wanapiga pasi nyingi.

Mchezo umeanza kwa kasi ya kawaida.

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza kwa kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 1 ya nyongeza.

Dakika ya 35: Chirwa anapata nafasi nzuri ya kufunga lakini shuti lake linambabatiza beki wa Tusker na kutoka nje.

Dakika ya 30: Yanga wanafanya shambulizi kali langoni mwa Tusker lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 25: Yanga wanajaribu kufanya mashambulizi kwa kumtumia Chirwa lakini anabanwa na wapinzani mara kadhaa.  Mchezo una kasi kwa pande zote.

Idadi ya watu ni wengi kiasi lakini bado sehemu nyingi za jukwaa zipo wazi.

Dakika ya 20: Mchezo umebalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 15: Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anawalalamikia wenzake kutokana na kufanya makosa.

Dakika ya 10: Mchezo unaendelea kwa kasi, inavyoonekana Yanga wanataka kumaliza kazi mapema na kutosubiri hatua ya penalti.

Dakika ya 7: Mchezo unaendelea kwa kas.

Huu ni mchezo wa michuano ya SportPesa Super Cup kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mchezo umeshaanza na sasa ni dakika ya 5 matokeo bado ni 0-0.