Home Michezo Yanga Kumkosa Ngoma kwa Muda Usiojulikana

Yanga Kumkosa Ngoma kwa Muda Usiojulikana

68
0

 

donald-Ngoma

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Yanga Donald Ngoma ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda usiojulikana baada ya kuumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar  na jana asubuhi Oktoba 2 akashindwa kuendelea na mazoezi.
Msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema kuwa bado wanasubiri ripoti ya daktari wa timu Dr. Edward Bavu ili kujua ni muda gani Ngoma atakaa nje.
Dismas ameongeza kuwa daktari Bavu amethibitisha kuwa ripoti hiyo inaweza kutoka ndani ya saa 48 zijazo baada ya kumfanyia uchunguzi wa kina nyota huyo raia wa Zimbabwe.
Donald Ngoma alishindwa kufanya Mazoezi asubuhi ya jana kufuatia maumivu misuli ya paja aliyoyapata kwenye mchezo uliopigwa Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo timu hizo zilitoka sare. Mchezo wa Yanga unaofuata utakuwa dhidi ya Kagera Sugar tarehe 14/10/2017 Kwenye uwanja wa Kaitaba.

Leave a comment