YANGA WAMNG'OA HUYU KUTOKA AZAM WAMLAMBISHA KANDARASI YA MIAKA MIWILI - The Choice

YANGA WAMNG’OA HUYU KUTOKA AZAM WAMLAMBISHA KANDARASI YA MIAKA MIWILI

0

Gadiel Michael kulia.

BEKI wa kushoto wa Azam FC, Gardiel Michael Mbaga amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC, lakini itabidi atasubiri hadi mzunguko wa pili kuanza kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Garidel anamaliza mkataba wake Azam FC Desemba mwaka huu, maana yake atalazimika kusubiri hadi mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ndio aanze kucheza, vinginevyo klabu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ifanye hisani.
Lakini kutokana na Gardiel kuzifanya taarifa hizo kuwa siri, inaonekana uongozi wa Azam hautakuwa tayari kumsikiliza zaidi ya kufuata taratibu, yaani asubiri hadi amalize mkataba.
Gardiel Michael amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC
Gardiel ni miongoni mwa wachezaji waliopatikana kutokana na sera nzuri za uwekezaji kwenye soka ya vijana ndani ya Azam FC pamoja na akina Aishi Manula anayekwenda Simba, Mudathir Yahya anayekwenda Singida United na Farid Mussa anayecheza kwa mkopo DC Tenerife ya Hispania.
Na baada ya kusaini Yanga kufuatia kutemwa kwa Oscar Joshua, Gardiel atakwenda kupambana kujaribu kumpindua beki chaguo la kwanza wa timu hiyo, Mwinyi Hajji Mngwali.
Wakati huo huo: Kiungo Mudathir Yahya naye amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili, kufuatia kumaliza mkataba wake Azam FC.  Uongozi wa Azam umetoa baraka zake zote kwa Mudathir kuhamia Singida.
Facebook Comments
Share.

About Author