Home Michezo Yanga watatua Utata wa Obrey Chirwa kama Atacheza dhidi ya Azam au...

Yanga watatua Utata wa Obrey Chirwa kama Atacheza dhidi ya Azam au La.

279
0

Kwasasa moja kati ya mijadala inayoendelea katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga kutoka nchini Zambia Obrey Chila Chirwa juu ya hatma yake ya kucheza kuelekea mchezo kati ya Azam Fc na Yanga Jumamosi Hii January 27.

Chirwa ambaye alifungiwa na TFF kutokana na kumpiga mchezaji wa Prisons kwenye mchezo kati ya Yanga na Tanzania Prisons uwanja wa Chamazi imeelezwa na Uongozi wa Yanga kuwa atacheza katika mchezo huo.

Akizungumza  mwenyekiti wa kamati ya Mashindano na mwenyekiti wa kamati ya Usajili Hussein Nyika amesema kuwa ni kweli Chirwa atacheza katika mchezo huo.

” Ni kweli Chirwa atakuwa anarejea katika mchezo kati ya Azam na Yanga kwani atakuwa amemaliza adhabu yake lakini hii ni endapo tu Mwalimu atampanga, Mwalimu akiona anafaa  kucheza basi atacheza “

Kukosekana kwa Obrey Chirwa kumekuwa kunaonekana pengo la wazi hasa kutokana na wachezaji waliopo kushindwa kuipatia Yanga magoli kama ambavyo Chirwa amekuwa Akifanya.

Kurejea kwa Amis Tambwe bado anaonekana kuwa hajawa fiti asilimia mia kama Tambwe wa msimu uliopita kwahiyo kurejea kwa Obrey Chirwa kunaweza kukaimarisha kwa kiasi Kikubwa safu ya Ushambuliaji ya Yanga na kurudisha imani ya washabiki kwenye safu ya Ushambuliaji ya Timu hiyo

Leave a comment