Yanga yaandamwa na majeruhi, Himid Mao aomba radhi - The Choice

Yanga yaandamwa na majeruhi, Himid Mao aomba radhi

0

Klabu ya Yanga imekiri kuathiriwa na majeruhi yanayozidi kuongezeka katika kikosi chake, lakini imejipa moyo kuwa majeruhi siyo mwisho wa mbio zake za kuutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania.

Kocha Mkuu wa klabu hiyo George Lwandamina ametoa kauli hiyo baada ya kiungo wake Justine Zulu kuchezewa rafu mbaya na Himid Mao Mkami wa Azam FC katika mchezo wa jana na kupelekea kiungo huyo kushonwa nyuzi tisa, ambapo amesema kuwa ongezeko la majeruhi lina athari kubwa katika kikosi chake.

“Hizi ni ajali za kawaida michezoni lakini zina athari kubwa kwa timu katika mipango yake na mchezaji husika katika kipaji chake na afya. Ni ukweli usiopingika majeruhi yanaleta athari kubwa kwenye timu yangu maana wachezaji wote wana mchango wao katika kuhakikisha timu inafikia malengo yake katika michuano yote tuliyopo. Tutaisikiliza ripoti ya daktari na kujua nini cha kufanya lakini bado tuna kikosi kipana kupambana”. Alisema Lwandamina

Kwa upande mwingine Mao baada ya mchezo huo kumalizika aliomba msamaha kwa alichokifanya kupitia mtandao wa kijamii akidai kuwa halikuwa kusudio lake kufanya hivyo.

“Nampa pole mchezaji wa Yanga Justine Zulu kwa kuumia, haikuwa nia yangu kumuumiza ni bahati mbaya, pia nilienda kumpa pole ‘halftime”.Alimeandika Mao kupitia twitter

Ikumbukwe pia katika mechi ya nusu fainali kombe la Mapinduzi Zanzibar, Mao alimchezea rafu mbaya kiungo huyo raia wa Zambia na kumfanya akae nje ya uwanja takribani wiki tatu.

Facebook Comments
Share.

About Author