Home Michezo Yanga yaota bao la mapema

Yanga yaota bao la mapema

18
0

Wachezaji wa Yanga wameondoka na lengo moja la kupata bao la mapema dhidi ya Zanaco katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inahitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili katika mchezo huo ili kufuzu kucheza hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Zanaco jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’ alisema wanachokifikiria ni kufuzu kucheza hatua ya makundi katika Ligi ya mabingwa Afrika.

“Tunakwenda Zambia na mkakati wa kutoruhusu kufungwa, pia tuhakikishe tunapata bao la mapema ambalo naamini litatusaidia kuwachanganya washindani wetu,” alisema Canavaro.

Mshambuliaji, Saimon Msuva aliwatoa hofu mashabiki wao na kusisitiza timu yao kutotolewa na Zanaco katika mashindano hayo.

“Mtizamo wetu ni kucheza hatua ya makundi na si vinginevyo, kama walipata bao Dar es Salaam, sisi tutashindwaje kufunga Zambia, kila kitu kinawezekana,” alijinasibu winga huyo.

Kocha Juma Mwambusi alisisitiza benchi la ufundi limefanyia kazi mapungufu yaliyoonekana katika mchezo wa awali na kusisitiza kwamba wanakwenda Zambia kushinda na si vinginevyo.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kitwana Manara alisema ni rahisi Yanga kuitoa Zanaco endapowatatulia na kucheza kitimu.

“Bahati nzuri mechi hiyo haitakuwa na presha kubwa kwa Yanga kama itakavyokuwa kwa Zanacoambayo hiko nyumbani, watulie, wacheze mpira nafasi ya kushinda ipo,” alisisitiza Manara.