“Zitto hafai kuiongoza TFF, ni mbinafsi” – Jerry Muro - The Choice

“Zitto hafai kuiongoza TFF, ni mbinafsi” – Jerry Muro

0

Siku za hivi karibuni kumeibuka stori ambayo imekuwa ikimake headlines kwenye mitandao mbalimbali hasa katika medani ya soka la Tanzania ikimuhusu Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kutaka kugombea Urais wa TFF.

Habari hiyo imekuwa ikiwagusa watu wengi ambapo miongoni mwao ni aliyekuwa Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro ambaye alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya hilo alisema Mbunge huyo hafai.

Akijibu swali la mtangazaji wa Clouds 360 ya Clouds TV, April 29, 2017 Jerry Muro ametoa mtazamo wake huo baada ya kuulizwa kama Zitto Kabwe atafaa kugombea Urais wa TFF akisema Zitto Kabwe hafai kuiongoza TFF kwa sababu ni mbinafsi ambaye alishindwa kukaa na wenzie akaenda kuanzisha chama chake binafsi.

“Hapana! Hawezi kuiongoza. Zitto ni mwanasiasa ambaye anatazama maslahi yake, hatazami maslahi ya watu wengine. Hafai kuiongoza TFF kwa sababu ni mbinafsi, ni mmimi. Kama mtu ameshindwa kukaa na wenzie akaamua kwenda kuanzia chama chake akiongoze mwenyewe ni mbinafsi.” – Jerry Muro.

Facebook Comments
Share.

About Author