Alexis Sanchez ndiye mchezaji bora kombe la Copa America - The Choice

Alexis Sanchez ndiye mchezaji bora kombe la Copa America

0

Mchezaji wa timu ya taifa ya Chile na klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez amefanikiwa kuibuka kuwa mchezaji bora kwenye mashindano ya Copa America yaliyomalizika alfajiri ya Jumatatu kwenye uwanja wa MetLife mjini New Jersey baada ya mchezo wa fainali kati ya Chile na Argentina.

sanches

Mashindano hayo yalikuwa yakifanyika nchini Marekani na kushuhudia Chile wakifanikiwa kunyakua kombe hilo kwa kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 na kuweka rekodi ya kuifunga timu hiyo ya Argentina mara ya pili mfululizo kwenye mchezo wa fainali ya kombe hilo.

Aidha Sanchez ndiye mchezaji aliyechezewa faulo nyingi zaidi kwenye mashindano hayo [Copa America] kwa mwaka huu lakini amefanikiwa kufunga magoli mawili na kutoa pasi tatu za mwisho zilizozaa magoli muhimu kwa Chile.

Kupitia akaunti ya twitter ya klabu yake ya Arsenal imeandika: “#CopaAmerica Player of the Tournament: Congratulations [email protected]_Sanchez!.” Hata hivyo Sanchez alikuwa akicheza na majeraha kwa muda mrefu kwenye mashindano hayo huku kwenye mchezo huo wa fainali alitolewa dakika ya 104 kutokana na kushindwa kuendelea na mchezo huo.

Share.

About Author