Alichokijibu Nsajigwa kuhusu sababu za Kumpanga Chirwa dhidi ya URA - The Choice

Alichokijibu Nsajigwa kuhusu sababu za Kumpanga Chirwa dhidi ya URA

0

Alichokijibu Nsajigwa kuhusu sababu za Kumpanga Chirwa dhidi ya URA

Yanga jana wamekubali kichapo kwenye matuta dhidi ya URA na kujikuta wanatolewa kwenye michuano ya Mapinduzi kwenye hatua ya nusu Fainali baada ya kufungwa penati 5 kwa 4.

Huku Yanga wakikosa penati moja iliyopigwa na Obrey Chirwa, huku waliopata wakiwa ni Tshishimbi, Kessy Raphael Daudi na Gadiel Michael.

Gumzo lililoibuka baada ya mchezo huo lilikuwa ni suala la mwalimu Nsajigwa Kumpanga Obrey Chirwa aliyeingia kipindi cha pili dakika ya 53 kuchukua nafasi ya Pius Buswita huku Chirwa akionekana wazi kukosa Utimamu wa mchezo (Match Fitness) na kuonekana kuanguka ovyo, kupiga pasi mbovu, kupiga mashuti yasiyo na Nguvu, kukosa kasi yake na mambo kama hayo.

Watu wengi wanahoji sababu ya kumpanga mchezaji huyo ambaye ni alikosekana kwenye kikosi cha Yanga baada ya kwenda kwao kwenye mapumziko mafupi na kisha mchezaji huyo kukaa zaidi hata ya muda ambao alitakiwa kukaa huku ikidaiwa kuwa mchezaji huyo aligoma kurejea Yanga mpaka atakapolipwa pesa zake za Usajili alizokuwa akiwadai Yanga

Na Jana (Siku ya mchezo)  baada ya kila  kitu kukaa sawa alijiunga na wenzake akienda Zanzibar na kocha Mkuu George Lwandamina

KOCHA NSAJINGWA ANASEMAJE JUU YA KUMPANGA OBREY CHIRWA?

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa akizungumza baada ya mchezo  amesema hayo masuala ni masula ya benchi la ufundi na hawezi kuyaongelea kwa sasa.

” Hayo ni masuala ya benchi la Ufundi siwezi kuyaongelea hapa, Kifupi ni mchezaji wetu hakuwepo ila maerejea tukaona tumtumie. “

Hata hivyo  siku moja kabla ya mchezo Kocha huyo msaidizi alisema kuwa hana mpango wa kutumia mchezaji mwingine nje ya wale ambao alienda nao Zanzibar.

Share.

About Author