Baada ya kudaiwa kutapeliwa na beki Mkongo, Yanga wazungumza Haya - The Choice

Baada ya kudaiwa kutapeliwa na beki Mkongo, Yanga wazungumza Haya

0

Baada ya kudaiwa kutapeliwa na Mkongo Fiston, Yanga wazungumzia

Mara baada ya Klabu ya Yanga kudaiwa kutapeliwa na Beki kutoka Nchi ya Congo Fiston Kayembe hatimaye Uongozi wa Yanga umeibuka na kukanusha Taarifa hizo ambazo zimekuwa zikizagaa sana kwenye vyombo vya habari.

Klabu ya Yanga   kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya Usajili na Mmoja ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya Klabu ya Yanga Hussein Nyika amesema si kweli kwamba wametapeliwa na Mchezaji huyo.

” Fiston Kayembe ni mchezaji wa Yanga alienda kwao kwaajili ya matatizo ya kifamilia  na siku yoyote atarejea nchini mara baada ya kukamilisha matatizo yaliyokuwa yanamkabili huko kwao na siyo kweli kuwa ametukimbia “

Nyika alikumbushia pia kuwa mchezaji huyo angekuwa tapeli asingekuja kukaa Tanzania kufanya majaribio ambapo alikaa wiki kadhaa akifanya majaribio na kufanikiwa kucheza mchezo mmoja wa Kirafiki akiwa na Jezi ya Yanga.

Nyika  amesema Kilichobakia ili mchezaji huyo kuvaa jezi ya Yanga ni mambo amdogo tu ya kiutawala na watu wategemee kumuona Fiston Kayembe wakati wowote ule ndani ya Yanga.

Washabiki, wadau, wapenzi na wanachama wengi wa Yanga walizua Hofu mara baada ya kutangaziwa kuwa mchezaji huyo amesaini Yanga lakini hawakuwa wakimuona katika kikosi cha Timu hiyo kabla ya baadhi ya vyombo vya Habari kuanza kusema kuwa Yanga wametapeliwa na Mkongo huyo ambaye anacheza nafasi ya Beki wa Kati.

1,631 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author