Baada ya kumtaka Kapombe aondoke Simba,Hanspope sasa anakauli hii kwa Kapombe baada ya kurejea kwa kasi - The Choice

Baada ya kumtaka Kapombe aondoke Simba,Hanspope sasa anakauli hii kwa Kapombe baada ya kurejea kwa kasi

0

November 13 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspoppe aliibuka na kutoa kauli ya kumtaka Shomari Kapombe aliyekuwa majeruhi kumtaka kama hataki kucheza basi aondoke katika Klabu ya SIMBA.

Katika kauli za Hanspoppe alikuwa anaamini Kapombe kashapona lakini hakuwa tu anataka kurejea uwanjani kwa sababu zake Binafsi, Hanspoppe alisema

“Vipimo havidanganyi, yeye kama anaona hawezi kucheza basi akae pembeni, siyo anakaa anakula mshahara wa bure.

“Kama amepona acheze, kama hataki basi aondoke, majeruhi gani ambaye haponi muda wote huo!”

Alipoulizwa kuhusu vipimo vinavyosema, alisema: “Vipimo vinaonyesha ameshapona vizuri, yeye ana uwoga wake tu, labda anaogopa ataumia, msimamo wetu ni yeye mwenyewe aamue acheze au aondoke.”

Lakini hapo juzi kati baada ya Kapombe kurejea juzi katka mchezo kati ya Kagera na Simba mchezo ulioisha kwa Simba kushinda bao 2 kwa 0 huku Kapombe aliyeingia kipindi cha Pili akirejea  vizuri kwa kutoa Pasi ya Goli la Pili lililofungwa na John Bocco.

Hanspoppe   amesema Kauli yake ilimsaidia Kapombe Kurejea kwani kisaikolojia Kapombe hakuwa anaamini kama atapona kwahiyo kauli yake Ilimsaidia kujipanga na kuchukua hatua madhubuti kurejea Uwanjani.

” Kisaikolojia mtu anaweza akawa anaamini kuwa ugonjwa alionao hawezi kupona kumbe unaweza ukapona na mara nyingi  kama hauamini na ukikosa imani kuwa utapona hata kwa daktari huwezi kupona “

Hanspoppe aongelea Kiwango chake

Hanspoppe amesema kuwa kiwango cha Shomari Kapombe anajua kuwa ni kiwango kikubwa ndiyo maana walimsajili katika klabu ya Simba.

” Najua kiwango chake ni kizuri ndiyo maana tulimsajili, Na nilijua atapoteza kipaji chake kama ataendelea kutokucheza  “

Alisema Hanspoppe

Share.

About Author