BEKI SIMBA APATA AJALI YA BODABODA NA KUSHINDWA KUSAFIRI NA TIMU HADI MISRI - The Choice

BEKI SIMBA APATA AJALI YA BODABODA NA KUSHINDWA KUSAFIRI NA TIMU HADI MISRI

0

 

Wakati Simba ikijiandaa kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry mjini Port Said, beki wa timu hiyo, Salim Mbonde ameshindwa kuondoka na timu baada ya kupata ajali ya pikipiki.

Beki huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji walikuwepo katika mipango ya Kocha Mkuu, Pierre Lechantre kumtumia katika mchezo huo kutokana na ajali hiyo iliyosababisha ashonwe nyuzi tatu juu kidogo ya jicho lake, amemuondoa katika mipango hiyo.

Baada ya ajali hiyo Mbonde alipokea taarifa kutoka kwa Daktari wa timu hiyo Dk Yassin Gembe kuwa hatokuwepo katika mchezo huo kutokana kuwa na majeraha hayo aliyoyapata na kusababisha kushindwa kuendelea na mazoezi ndani ya kikosi hicho

Simba inahitaji ushindi wowote au sare ya magoli 3-3 ili kusonga mbele, hiyo inakuja baada ya sare ya magoli 2-2 katika mchezo wa wa awali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa-Dar es Salaam wiki iliyopita.

Kikosi kamili kinachosafiri kwenda Misri ni

1.Aishi Salum Manula

2.Said Mohamed’Nduda’

3.Yusufu Mlipili

4.Juuko Murushid

5.Shomari Salum Kapombe

6.Said Hamisi Ndemla

7.Mohamed Hussein JR

8.Asante Kwasi

9.Erasto Edwars Nyoni

10.Mzamiru Yassin

11.Jonas Gerald Mkude

12.John Raphael Bocco

13.Paul Bukaba

14.Mwinyi Kazimoto

15.Shiza Ramadhan Kichuya

16.Nicholas Gyan

17.Laudit Mavugo

18.James Kotei

19.Emanuel Anord Okwi

20.Juma Luizio ‘Ndanda’

Viongozi wanaosafiri

1.Pierre lichantre

2.Masoud Djuma

3.Muharam Mohammed

4.Mohammed Aymen

5.Dr Yassin Gembe

6.Richard Robert (Team Manager)

7. Yassin Mtambo (Kit Manager)

Mkuu wa Msafara ni Kaimu Rais wa Simba Dr Salim Abdallah

Share.

About Author