Home News BODI YA WAKURUGENZI TANESCO YATEMBELEA KATAVI

BODI YA WAKURUGENZI TANESCO YATEMBELEA KATAVI

851
0

Baadhi ya matenki ya mafuta yanayotumika kuendesha mitambo hiyo ya kufua umeme mkoani Katavi.

 

Mitambo ya kufua umeme iliyopo  mjii Mpanda mkoani Katavi.
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Katavi
Bodi Ya Wakurugenzi Ya Shirika La Umeme Nchini (Tanesco) Imefanya Ziara Ya Siku Moja Mkoani Katavi Kwa Lengo La Kukagua Mashine Za Kuzalishia Umeme Pamoja Na Kutambua Changamoto Mbalimbali Zinazohusiana Na Utoaji Wa Huduma Ya Nishati Ya Umeme Katika Mkoa Huo
Akizungumza Na Wafanyakazi Wa Tanesco Mkoa Wa Katavi; Makamu Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi Ya Tanesco Balozi James Nzagi Amewataka Wafanyakazi Kujituma Kufanya Kazi Kwa Bidii Na Kupata Wateja Wa Kutosha
Ameongeza Kuwa Dhamira Ya Shirika Ni Kuwa Na Zaidi Ya Megawati 5000 Hali Itakayowezesha Uendeshaji Wa Tanzania Ya Viwanda  
Kwa Upande Wake Meneja Wa Tanesco Mkoa Wa Katavi Bwana Felix Olang Amesema Kwa Sasa Shirika Limeshindwa Kuunganisha Zaidi Ya Wateja 15,000 Kutokana Na Kuwa Na Mashine Chache Za Kufua Umeme
Ametaja Mashine Hizo Kuwa Tatu Ziko Katika Manispaa Ya Mpanda Na Zina Uwezo Wa Kuzalisha Megawati 3.7 Na Moja Iko Inyonga Wilaya Mlele Yenye Uwezo Wa Kuzalisha Umeme Kilowati 420
Bwana Olang’ Amesema Hali Hiyo Imepelekea Kuwa Na Mteja Mkubwa Mmoja Tu Ambaye Ni Mamlaka Ya Maji Safi Na Maji Taka  (Muwasa); Huku Wakishindwa Kuunganisha Wateja Walio Katika Migodi Ya Madini mbalimbali Ya Dhahabu Na Madini Ya Ujenzi
Pia Ameiomba Bodi Kuangalia Katavi Kwa Jicho La Pekee Kuiongezea Mashine Pale Zinapopatikana Kwani Katika Mikoa Mingine Kuna Mashine Za Ziada
Awali Mjumbe Wa Bodi Hiyo Bwana David Alal Amesema Baadhi Ya Mikoa Ambayo Haijaunganishwa Na Umeme Wa Gridi Ya Taifa Inakabiliana Na Changamoto Mbalimbali Za Uendeshaji Wa Vituo Vya Uzalishaji Umeme
Amesema Licha Ya Changamoto Hizo Watumishi Wa Shirika Hilo Wanapaswa Kuwa Mstari Wa Mbele Katika Kuhudumia Wateja Na Kukwepa Kashfa Kama Za Lugha Chafu Na Rushwa Ili Kuwezesha Shirika Kufanikiwa Kujitegemea
“Tukiwahudumia Vizuri Tutaongeza Wateja, Tukiongeza Wateja Mapato Yataongezeka” Alisema Alal.

Wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Katavi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo alipofanya ziara mkoani Katavi leo

Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo balozi James Nzagi akizungumza jambo mbele ya wajumbe wenzake na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Katavi.

Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO wakishuka katika moja ya mashine ya kufua umeme. Aliyeko mbele ni meneja wa TANESCO mkoa wa Katavi Felix Olang’

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wakikagua Mita za kupima matumizi ya umeme. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo balozi James Nzagi