AFRIKA KUSINI: Rais Jacob Zuma amekubali kuachia madaraka ya kuongoza nchi hiyo, baada ya wito uliotolewa na chama chake ANC kumtaka kujiuzulu ndani ya masaa 48
–
Makubaliano hayo ya kujiuzulu yamekuja na sharti kwamba atafanya hivyo baada ya miezi 3 mpaka 6 kuanzia sasa. Bado uongozi wa ANC haujatoa jibu kama umeridhia ombi hilo.
–
Rais Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa uongozi wa chama tawala (ANC) Desemba mwaka jana
–
Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo
2,429 total views, 4 views today
Facebook Comments