Chirwa afunguka Ishu ya Kutaka Milioni 150 Yanga na Ya Kugoma kwenda SheliSheli - The Choice

Chirwa afunguka Ishu ya Kutaka Milioni 150 Yanga na Ya Kugoma kwenda SheliSheli

0

Chirwa afunguka Ishu ya Kutaka Milioni 150 na Ya Kugoma kwenda SheliSheli

Mshambuliaji wa Timu ya Yangfa Obrey Chirwa amekanusha Vikali suala linalosemwa na Baadhi ya vyombo vya Habari kuwa anahitaji milioni 150 ili aweze kusaini mkataba mpya mpya Yanga.

Chirwa pia amekanusha taarifa za Kukataa kwenda na Timu Shelisheli huku akisisitiza Kuwa yeye hajaenda kutokana na Kuwa na Maumivu ya Misuli aliyoyapata wakati wa mechi ya Yanga na Maji Maji.

Kupitia Ukurasa wa Twitter wa Yanga  wamenukuu maneno ya Obrey Chirwa akiongelea Taarifa Hizo.

“Sijawahi kusema popote nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia,nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.
Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuuzi,mimi ni mchezaji wa Yanga”. – OBREY CHIRWA

Share.

About Author