CHIRWA AZUA GUMZO MTANDAONI NI BAADA YA KUWEKA HII PICHA - The Choice

CHIRWA AZUA GUMZO MTANDAONI NI BAADA YA KUWEKA HII PICHA

0

V

Wakati kukiwa na habari za chini kwa chini kuwa Mchezaji anayecheza nafasi ya Ushambuliaji Yanga Obrey Chrwa kuwa amegoma kurejea kituo chake cha Kazi ndani ya klabu ya Yanga hali imezidi kuonekana ngumu.

Chirwa amepost picha akiwa kwao akiwa Shambani akifanya palizi kwenye mahindi huku akiwa ameandika caption ya Chirwa C Basi, bila hata kutoa maelezo.

Picha hiyo inatafsiriwa tofauti na watu wengi ambao walimtegemea mchezaji huyo kuwa kwenye kikosi cha Yanga muda Huu lakini hajaonekana na inasemekana kagoma mpaka atakapolipwa malimbikizo yake anayowadai Yanga.

Chirwa amekuwa tegemeo kubwa msimu huu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga akisaidiana Ibrahim Ajibu alitegemewa kuonekana jana Yanga wakicheza dhidi ya Reha fc lakini mambo hayakwenda Hivyo kwani hakuwepo kwenye kikosi na hata benchi.

Picha aliyopost ChirwaKisha baada ya mechi hiyo baadaye akapost picha Mbili akiwa shamba hali inayotafsiriwa kama hana mpango vile na Yanga na badala yake ameamua kujikita kwenye kilimo huku baadhi ya washabiki wakiona kuwa hajatua nchini ili amalizie tu palizi yake ya mahindi, Wengine wakiamini ni wakati wa likizo kwahiyo labda atarejea baada ya sikukuu.

Hata hivyo Uongozi wa Yanga bado haujatoa taarifa rasmi juu ya taarifa za Chirwa kutoonekana nchini mpaka sasa.

Share.

About Author