Diamond atangaza ujio wa Wasafi FM na Wasafi TV - The Choice

Diamond atangaza ujio wa Wasafi FM na Wasafi TV

0

Rais wa WCB, Diamond Platnumz ametangaza habari njema kwa watanzania hasa hasa kwa wadau wa tasnia ya habari kwamba anatarajia kufungua Wasafi FM na Wasafi TV
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waka’ akiwa amemshirikisha msanii wa muziki wa kufoka kutoka Marekani, Rick Ross, alitoa taarifa ya ujio wa redio hiyo na TV jana kupitia kipindi cha #10over10 cha Citizen Tv Kenya.
[​IMG]
Hata hivyo kabla ya jana ku confirm ujio huo wa redio na Tv lakini pia Diamond Platnumz kupitia twitter yake Disemba 30 mwaka 2017 alitoa taarifa hio lakini muda mfupi baadae aliifuta taarifa hiyo.
[​IMG]

Share.

About Author