Diamond Platnumz, Ababuu, Msami na Jaquar Walishatoka na Irene Uwoya..Mumewe Afichua Siri - The Choice

Diamond Platnumz, Ababuu, Msami na Jaquar Walishatoka na Irene Uwoya..Mumewe Afichua Siri

0
UWOYA-1

Aliyekuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana kutoka nchini Rwanda amefunguka mambo kibao ya moyoni kuhusu ndoa yake na mrembo huyo ambapo kwa sasa ameweka wazi dhamira yake ya kumpa talaka.

Ndikumana ametumia mtandao wa Instagram kueleza madudu yote yalikuwa katika ndoa yake huku akiwataja wasanii maarufu kuingilia ndoa yake.

Unasema sina aibu kuandika hayo mitandaoni, wewe uliona aibu kuwa kwenye mahusiano na msami mnyaka miwili ukiwa ndani ya ndoa ? mara ngapi nilikuuliza kuhusu huyo mtu ukalala chini eti uongo ? Mara ngapi nilikuuliza kuhusu kulala na Diamond ukaapa kufa ? ila mwisho wa siku mwenyewe kasema kwanini ilifanya vile. Mimi kama mjinga nilikutetea sana tena baada yako kuwaambia magazeti eti nimezimia kitu ambacho sijawahi kukanusha ila leo nakikanusa sijawahi kuzimia maishani mwangu…

Irene unakumbuka nilikuwa nilivyokuwa taabaaani karibu kufa huku upo mozambike unatanua na Ababuu hata ujali nataka kufa ? Na uliporudi hata ukutaka kuniona,but sikushaanga kwavile nilikuwa najua wewe ndo uliyofanya yote.ulikuja Rwanda kuniona baada ya kuondoka siku mbili yakaja ya JAGUAR ?…

Hayo ni machache kati ya mengi mno aliyoandika Ndikumana, wawili hao walifunga ndoa mwaka 2009 wakati mchezaji huyo akicheza soka hapa nchini, katika ndoa yao wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwae Krish.

Share.

About Author