Home Michezo Dongo la Dismas Ten kwa Haji Manara baada ya Yanga kuifunga USM...

Dongo la Dismas Ten kwa Haji Manara baada ya Yanga kuifunga USM Alger

2580
0

Dongo la Dismas Ten kwa Haji Manara baada ya Yanga kuifunga USM Alger

Kuna muda soka huwa unakuwa mchezo ambao siyo wa uwanjani tena na hasa linapokuja suala la Tambo za hapa na pale.

Kila mmoja hususani mpenzi wa soka nchini anajua maneno ya Haji manara hasa Simba inapokuwa imefanya Vizuri na Yanga ikazingua.

Sasa Dismas Ten mara baada ya Ushindi wa Yanga dhidi ya USM Alger wa bao 2 kwa 1 aliamua kumtupia dongo la chini chini Msemaji wa Simba ambaye amekuwa haishiwi cha kupost kila Yanga inapoteleza.

 

Kupitia ukurasa wa Instgram Dismas Ten aliuliza swali Hivi wamepost au bado, na Kisha akaandika hashtag ya au bando limeisha ikiwa ni kama ujumbe kwa Haji Manara ambaye hakupost chochote baada ya Ushindi wa Yanga.

Eti..! Hivi wamepost au bado..! #aubandolimeisha?