EXCLUSIVE: KESSY RASMI LEO ANATUA YANGA, ANASAINI NA KUPEWA JEZI YAKE - The Choice

EXCLUSIVE: KESSY RASMI LEO ANATUA YANGA, ANASAINI NA KUPEWA JEZI YAKE

0
kessy2
Kilichobaki kati ya Yanga na beki Hassan Kessy ni kuweka saini kwenye mkataba pekee.
Yanga na beki huyo ambaye mkataba wake Simba unakwisha, wamefikia mwafaka baada ya kukubaliana kila kitu na leo matarajio makubwa atasaini rasmi na kuwa mchezaji wa Yanga.
Si unakumbuka Kessy aliomba apewe jezi namba 25 iliyokuwa inavaliwa na Emmanuel Okwi. Sasa huenda akakabidhiwa leo rasmi.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimesema baada ya kuona hana uhakika wa kubaki Msimbazi, Kessy amefanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na wamemalizana kwa kuwa mkataba wake Simba, ‘umeisha’.
“Nakuambia kila kitu kati ya Yanga na Kessy kimeisha. Suala la kusaini ndiyo lilikuwa halijakamilika, ila Ijumaa, mambo yote yanakamilika na Kessy anasaini kuanza kuichezea Yanga,” kilieleza chanzo.
Kessy amekiri kufanya mazungumza na Yanga pia.
“Kweli lakini nafikiri meneja wangu ndiye anaweza kulizungumzia hilo,” alisema.
Alipotafutwa meneja wake, Tippo Athumani ‘Zizzou’ ambaye ni kiungo wa zamani wa Milambo ya Tabora na Coastal Union, pia alikubali.

 

“Kweli tuko katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Lakini vizuri tukimaliza, tunaweza kuwaeleza kila kitu,” alisema Tippo.
Share.

About Author